YANGA NA SIMBA 1-1

0
78

MPIRA UMEKWISHAAAAAA
Dk 90+1 Yanga wanapata kona baada ya Nyoni kuokoa wakati akimzuia, Ajibu anakwenda kuichonga

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 89 Chirwa yuko chini pale, aliutoa mpira nje na kukaa chini, inaonekana ameumia, anatolewa kutibiwa
Dk 88 Bocco anaingiza krosi nzuri, kabla ya mpira haujamfikia Okwi, Rostande anaruka vizuri na kuokoa
Dk 87 Yondani yuko chini baada ya kuminya na kiatu cha Bocco, anatolewa kwenda kutibiwa nje
Dk 86 Niyonzima anaachia mkwaju mkali baada ya kugeuka vizuri, goal kick
SUB Dk 84 Simba wanamtoa Muzamiru na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla, maana yake Simba wamemaliza Sub
Dk 81, Bocco anageuka mbele ya Yondani na kauchia mkwaju hapa, goal kick

Dk 78, Ajibu anaweka kifuani mbele ya Juuko, anapiga mkwaju lakini unakuwa nyanya
Dk 76 Kichuya anaunganisha krosi ya chinichini ya Niyonzima, goal kick
SUB Dk 75 Simba wanamtoa Kotei na nafasi yake inachukuliwa na Jonas Mkude
Dk 75, Simba wanagongeana vizuri, krosi nzuri ya Nyoni inakuwa kona nyingine
Dk 73 kona safi, kichwa kinapigwa safi, Simba wanaokoa katika msitari kabisa
Dk 72 Simba wanajisahau, Yanga wanafanya shambulizi la kushitukiza, Emmanuel Martin yeye na kipa, anaachia mkwaju hapa, Manula anapangua na kwua kona

KADI Dk 70, Juma Abdul analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Okwi
Dk 70 krosi nzuri ya Tshishimbi, Ajibu anaunganisha vizuri kifundi kabisa lakini mpira unatoka juu kidogo tu
KADI Dk 69, Ajibu analambwa kadi ya njano baada ya kuonyesha jazba baada ya mwamuzi kupuliza filimbi
Dk 67 Simba wanapata kona nyingine baada ya Okwi kuingia vizuri, inachongwa na Niyonzima, Rostande anaokoa vizuri kabisa
Dk 66 Simba wanafanya shambulizi jingine, Yanga wanaokoa,inakuwa kona. Inachongwa vizuri hapa, kichwa cha Bocco, goal kick
SUB Dk 65 Yanga wamatoa Raphael Daud na nafasi yake ianchukuliwa na mkabaji Pato Ngonyani
Dk 62 Mwashiuya anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin

GOOOOOOOOO Dk 60, Yanga wanasawazisha kupitia Chirwa baada ya pasi ya Ajibu kumfikia Gadiel ambaye kapiga krosi dongo na Chirwa anaunganisha mbele ya Juuko
KADI Dk 58 Kichuya analambwa kadi ya njano kwa kukimbia nje ya uwanja na kupoteza muda
GOOOOOOOOOOOOOOOO Dk 57 Kichuya anafunga baada ya kipa kupangua krosi ya Okwi, Nyoni anapiga krosi fupi
Dk 57 Bocco anaachia mkwaju mwingine mkali hapa, kipa anaokoa
Dk 56, Bocco anaingia na kuachia mkwaju mkali wa kwanza, Yanga wanaokoa
SUB Dk 56, Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mavugo nafasi yake inachukuliwa na John Bocco

Dk 55, Yanga wanafanya shambulizi la kushtukiza, shuti la MWashiuya, Manula anaokoa na kuwa kona

Dk 54, Gadel Michael anautoa mpira unakuwa ni kona, Simba wanachonga lakini Yanga wanaokoa
Dk 50 mpira wa adhabu wa Okwi unagonga ukyta wa walinzi wa Yanga, unaokolewa
Dk 49, Niyonzima anajaribu kuichambua difensi ya Yanga, anawekwa chini hapa na Juma Abdul, yuko chini pale anatibiwa. Ni eneo ambalo Okwi alifunga bao katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar
Dk 47, Mavugo anaingia vizuri lakini anapiga krosi mbovu kabisa
Dk 45 mpira umeanza kwa kasi kubwa na inaonekana utakuwa na presha kubwa kwa kuwa kila upande utataka kumaliza kazi mapema au katika kipindi hiki

MAPUMZIKO

DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45 krosi nzuri ndani ya lango la Yanga, Yondani anaruka na kuokoa na wachezaji Simba wanamkimbilia mwamuzi wakilalamika Yondani alishika
Dk 44, krosi nzuri ya Niyonzima lakini Okwi anashindwa kuiwahi na Vicent anaokoa vizuri
Dk 42 sasa, ukiangalia Yanga wanavyocheza katika hizi dakika utafikiri kuna timu moja inaongoza kwa mabao au inasubiri kufungwa ili icharuke na kurudisha bao hilo

Dk 40 sasa, zaidi mpira umechezwa katikati ya uwanja ikionekana kila upande unacheza kwa tahadhari
Dk 36 Ajibu anaonekana kuchukua kasi katikati ya uwanja, Kotei anamuweka chini
Dk 36 Niyonzima anamuacha Tshishimbi na kutoa krosi safi, Yondani anaokoa vizuri
Dk 35 Raphael analazimika kuachia mkwaju ambao haukulenga lango
Dk 33, pasi nzuri ya Niyonzima eneo la 18 ya Yanga lakini Mavugo ameshika
Dk 31, shambulizi jingine la Yanga, krosi safi safi ya Chirwa katikati ya lango la Simba lakini hakuna mwenyewe
Dk 30, Manula analazimika kufanya kazi ya kuikoa Simba baada ya shuti kali la Tshishimbi na kuwa kona. Inachongwa lakini ni kona dhaifu

Dk 28 Yondani anataka kufanya kosa, akisubiri mpira, Mavugo anauwahi na kutoa krosi lakini kipa Rostande anauwahi
Dk 27 pasi ndefu ya Niyonzima, Mavugo anauwahi mpira, anaingia na kuachia mkwaju, goal kick
Dk 24, Yanga wanafanya shambulizi jingine zuri, Manula anaokoa inakuwa kona ya kwanza ya Yanga. Inachongwa na Mwashiuya na kuokolewa

Dk 23, shambulizi kali wanafanya Yanga, shuti kali Mwashiuya, Manula anautema, Tshishimbi naye anaachia mkwaju mali hapa, goal kick
Dk 22, Simba wanagongeana vizuri Nyoni, Okwi, Kichuya na Nyoni anapiga kwisi safi lakini mpira wa kichwa wa Okwi, haukulenga lango

Dk 18, Okwi na Niyonzima wanagongeana vizuri lakini Yanga wako makini wanatoa na kuwa kona ya pili ya Simba, inachongwa lakini ni goal kick
Dk 14, Kichuya na Nyoni wanagongeana inakuwa ni kona, inachongwa lakini ni goal kick
Dk 12 mpira wa adhabu wa Ajibu unaishia miguuni mwa mabeki wa Simba
Dk 11, mwamuzi Sasi analazimika kuwaamua Chirwa na Juuko waliotaka kuzozana baada ya Juuko kuingia kuokoa na kumgonga Chirwa
Dk ya 10 sasa, mpira zaidi umechezwa katikati ya uwanja, Simba wakimiliki zaidi mpira

Dk 6, Yanga nao wanajibu, lakini pasi nzuri ya mwisho, Ajibu anakuwa ameotea ikiwa ni offside ya kwanza ya mchezo
Dk 5, Nyoni anamlamba chenga Juma Abdul na kuingia vizuri kabisa, krosi yake kipa Rostande anadaka vizuri kabisa
Dk 2, Yanga wanagongeana vizuri hadi katika lango la Simba lakini mpira unamzidi Buswita, goal kick
Dk 1, Simba wanagongeana tena haraka, Mavugo anauwahi mpira wa Kichuya na kuachia shuti tena, ni nyanya, goal kick
Dk 1, mpira umeanza na Simba wanakuwa wa kwanza kulianzisha gozri la ng’ombe, kwa spidi kali na kuingia kwenye lango la Yanga na Mavugo anaachia mkwaju mkuuubwa, goal kick

KIKOSI CHA YANGA:
1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrew Vicent
5. Kelvin Yondani
6. Papy Tshitshimbi
7. Pius Buswita
8. Raphael Daud
9. Obrey Chirwa
10. Ibrahim Ajibu
11. Geofrey Mwashiuya

KIKOSI CHA SIMBA:
1. Aishi Manula
2. Erasto Nyoni
3. Mohamed Zimbwe (C)
4. Juuko Murshid
5. Method Mwanjale
6. James Kotei
7. Shiza Kichuya
8. Muzamiru Yassin
9. Laudit Mavugo
10. Emmanuel Okwi
11. Haruna Niyonzima

NO COMMENTS