Wikileaks na China

0
368


Julian Assange.

Moja ya nyaraka za kidiplomasia zilizovuja zilimkariri afisa wa juu wa China akisema hali ya uchumi wa nchi hiyo imetengenezwa na hivyo si ya kutegemea.

Balozi wa zamani wa Marekani Clark Randt aliandika taarifa hiyo 2007 baada ya chakula cha jioni na naibu waziri mkuu wa China Li Keqiang ambaye kwa wakati huo alikuwa mkuu wa chama cha kikomunisti katika jimbo la kaskazini mashariki la Liaoning.

Ni miongoni mwa maelfu ya nyaraka zilizotolewa hivi karibuni na Wikileaks.Muasisi huyo wa Wikileaks ambaye sasa yuko Lupango alinyimwa dhamana na mahakama moja ya Uingereza kwa kosa la kubaka huko nchini Sweden ambako anatakiwa kwenda kujibu mashitaka.

Lakini hivi sasa Julian Assange anataka kupambana na kuzuia uwezekano wa kupelekwa Sweden kujibu mashtaka.

Chanzo:www.voanews.com

NO COMMENTS