Waziri wa mambo ya ndani Burundi asema rais Nkurunzinza amerudi nchini humo.

0
274

BREAKINGNEWS150513155644_rais_nkurunzinza_624x351_bbc_nocredit
Afisa wa juu wa Burundi anakanusha habari ya kupinduliwa kwa rais wa nchi hiyo na Jenerali muasi.

Waziri wa mambo ya ndani Edourd Nduwimana ameiambia Sauti ya Amerika kwamba majeshi yanayomuunga mkono rais Nkurunzinza bado yanadhibiti nchi ikiwa ni pamoja na ikulu ya rais, radio ya serikali na televisheni na uwanja wa ndege katika mji mkuu Bujumbura.

Amesema rais amesharudi Burundi kutoka safariNi Tanzania kwa ajili ya mkutano kuhusiana na mzozo katika kanda hiyo Jumatano ingawa hakusema alipo Bw.Nkurunzinza.

White house imetoa wito wa kuachwa kwa ghasia mara moja na pande zote kuweka silaha chini.Msemaji wa White House Josh Earnest pia ameunga mkono juhudi zinazoendelea za viongozi wa kanda kurudisha Amani na umoja katika nchi hiyo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema wanadiplomasia wa Marekani walizungumza na washauri wakuu wa rais mapema Jumatano.Lakini msemaji huyo amesema mazungumzo hayo huenda yalifanyika kabla ya madai ya mapinduzi kutolewa.

Mapema Jenerali Godefroid Niyombare aliiambia radio binafsi ya Burundi kwamba ras amepinduliwa na kusema kwamba ataunda kamati kurudisha Amani na umoja wa kitaifa.
Chanzo:VOA

NO COMMENTS