Waziri Mkuu kuhamaia Dodoma Septemba

0
231

Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA ameagiza mawaziri na manaibu mawaziri na watendaji wengine wa serikali kuanza mchakato wa kuhamia DODOMA mara moja

Akizungumza katika sherehe za mashujaa katika viwanja vya mashujaa mjini DODOMA Waziri Mkuu MAJALIWA amesema yeye atakuwa amehamia DODOMA itakapofika mwezi Septemba mwaka huu.

Waziri mkuu MAJALIWA amesema hatua ya serikali kuhamia DODOMAinatoa fursa kwa wakazi wa mkoa huo kupata vyanzo vya mapato.

Amewataka wakazi wa DODOMA kuboresha nyumba zao pamoja na kuongeza tija wakati ambapo serikali inapojipanga kuhamia mkoani humo.

Chanzo: TBC Newsimageimage

NO COMMENTS