Watanzania waibuka na Reality Show Growing up African.

0
364


Haya ni maelezo mafupi ya washiriki wa Reality Show ya watanzania waishio Marekani familia ya Lujwangana wakijitambulisha kwenu. Show ya “Growing Up African” ina onyesha familia kutoka Tanzania na maisha yao Marekani imeanza kutoa video. Mwezi wa Desemba kila wiki kutakuwa na Episode zitakazoonekana kwenye mtandao wao. (www.growingupafrican.com)

Episode ya kwanza inaonekana sasa hivi na tunawaomba watanzania wenzetu waangalie hizi episode ili show ziingie kwenye network nyingine. Kwenye hizi episode utakutana na ndugu wote kwenye familia hii kuanzia Bea, Eliza, Jessica, Johnson na Andrew ambao huwa maisha yao na tabia zao ni tofauti kwa kila mmoja. Episode nyingine zitakuwa na familia nzima ambayo utaona ile “family dynamic” ya ndugu wote.

Hapo hapo kutakuwa na vipindi mbali mbali kama vile P-Square wakiwa ndani ya New York City, na harusi kubwa ya ndugu na mambo ya mengine mengi ili watanzania wajionee maisha yalivyo hapa Marekani. Kutakuwa pia na mambo ya kitanzania yanayoendelea hapa kama Party ya watanzania kuadhimisha Uhuru iliyofanyika huko Washington DC na hotuba ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alipotembelea New York n.k.

Hii show kwanza, ni ya Watanzania na tungependa tuwasikie mnavyosema kabla ya kuwa kwenye soko la kimataifa (International Spotlight) na mashirika makubwa hapa Marekani. Mkitaka kuona hizo episode mnaweza kwenda kwenye youtube.com, bongo5.com au G5click.com chagua “Growing Up African kuona hayo mambo.

Tovuti sasa hivi iko tayari na ina mambo mengi sana kama mawazo ya familia kwenye masuala kama muziki, fashion, urembo, na vinginevyo vingi kwenye blog, mwezi wa Desemba utakuwa Introduction ya mambo ya show na bado tunaendelea kusikiliza maoni ya watu huko nyumbani na ndio familia itachagua shirika la kurusha Season ya kwanza. Familia itakwenda Tanzania mwakani, 2011.

Asanteni sana, na ninaomba ushauri na mawazo kutoka kwenu kama watanzania wenzetu. Kwa mwenye ushauri zaidi naomba ujisikie huru kuwasiliana nami kwa

Simu ya mkono: +1917 442 1822
Barua Pepe: lupembejames@yahoo.com

NO COMMENTS