Washiriki wa Dancing with the Stars waingia kambini

0
328
Kutoka kushoto Cherry Burke na Rick Fox,Bristol Palin na Maek Ballas na Jeniffer Grey na Dereck Hough
Kutoka kushoto Cherry Burke na Rick Fox,Bristol Palin na Maek Ballas na Jeniffer Grey na Dereck Hough

Baadhi ya washiriki wa ile show maaarufu Dancing with the stars ambao itaanza mwezi huu wa Septemba mshiriki mmoja wao Bristol Palin (kati kati) mtoto wa Gavana wa zamani wa Alaska Sara Palin amedai yeye atakuwa tofauti na washiriki wengine wote wa siku za nyuma kwani mavazi yake yatakuwa ni ya kutokuonyesha mwili wake kama watu wengi walivyozoea kuwaona kina dada katika show hiyo.

Naye mcheza Reality show maarufu Mike Sorentino “The Situation” wa Jersey Show anategemewa kuwa kivutio kikubwa na pengine kutoa upinzani wa hali ya juu kwenye show hiyo kwa utaalam wake wa kucheza na hasa ikizingatia ana kile kinachoitwa “six pack” ambayo kina dada wengi sana wanaipenda na amejipatia rundo la mashabiki kwa hilo.

Mike Sorrentino "The Situation"
Mike Sorrentino "The Situation"

Washiriki wengine wa show hiyo ni pamoja na Brandy Norwood,David  Hasselhoff (aliyecheza mlolongo wa TV Knight Rider) ambaye ni mcheza filam, mwimbaji na “prodyuza” halikadhalika mwimbaji mashuhuri wa “kuchombeza” Michael Bolton, Brandy na staa ambaye ni  kijana mdogo wa Disney Channel Kyle Massey, show hiyo inatarajiwa kuanza Septemba 20 na wananchi hapa Marekani wanaingoja kwa hamu. Vile vile Jenniffer Grey staa wa filamu  Dirty Dancing  na Brandy wanaonekana kuwa huenda wakaleta ushindani mkubwa na kuchukua maxi za juu kwenye mashindano hayo. Washiriki wengine katika orodha ni Florence Henderson ambaye ni mzee kuliko wote msimu huu (76), Audrina Patridge na  mchekeshaji Margret Cho.

Brandy
Brandy
David Hasselhoff
David Hasselhoff

NO COMMENTS