Wasanii Kigosi na Anti Ezekiel watangaza kurudi CCM.

0
3650

Anti EzekielZikiwa zimebaki takribani siku 39 kuelekea siku ya Kupiga kura. Wasanii wawili wa tasnia ya Maigizo waliokuwa katika Kampeni za Mh Edward Lowassa wa CHADEMA ghafla wameamia kwenye Kampeni za Mh John P. Magufuli wa CCM.

Hii imethibitishwa na mmoja wa wasanii hao, yaani Anti Ezekiel kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter. ( Auntezeofficial)

Ni stori ya kisiasa ambayo ilianza kuchukua headlines kwenye mitandao mbalimbali kuhusu wasanii wawili wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi aka Ray kuondoka UKAWA na kuhamia chama cha Mapinduzi.

Vincent-Kigosi

Baada ya taarifa hizo kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao sasa ripota wa millardayo.com amezungumza na Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kampeni ya Mama ongea na Mwanao…’Ndugu zetu wakina Vicent Kigosi na Aunt Ezekiel walitoroka wamerudi CCM kabla hawajatangaza lakini watatangaza wamerudi kwa kishindo kikubwa wanaamini bila hapo walipofika bila nguvu ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete wasingiweza kufika‘ – Steve Nyerere.

‘Kwa hiyo nataka kuwaambia watanzania kuwa hao watu wamerudi katika chama cha mapinduzi na wala msidanganywe pilika pilika za huku na kule hawa watu ni wanachama wa CCM hai walitoroka na sifa ya kutoroka ni kukosa nidhani kwa sisi wazazi ambao tuna watoto , mtoto akitoroka unatakiwa umpe adhabu ili siku nyingi afahamu njia ya sahihi na njia sahihi ni chama cha Mapinduzi ambacho kina Dkt John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu’ – Steve Nyerere.
Chanzo-Jamii Forum.

NO COMMENTS