Wanacahama 500 wa Chadema Ludewa watimkia ACT Wazalendo.

0
813Add caption

Wanachama  wa Chadema wilaya ya  Ludewa  mkoa wa  Njombe  wakiandamana  kupinga  maamuzi ya  chama  hicho  kukata  jina la mshindi  wa  kura  za maoni na  kumteua  aliyeshindwa ,mbali ya  kuandamana  pia  wanachama  hao  zaidi ya  500  walikihama  chama  hicho na  kujiunga na  ACT  Wazalendo

Wanachama  wa  Chadema  waliohamia ACT wazalendo  wakiwa na  mabango ya  kukituhumu  chama   hicho  kwa  kukiuka  Demokrasia


kadi na nyalaka  za Chadema  zikichomwa moto

Wanachadema  wakiwa  nje ya  ofisi ya  ACT  Wazalendo  ambako  walifika  kuomba  kujiunga huko

kadi  za  chadema  zikiteketezwa  kwa  motowana chadema  wakiwa na mabango

Hasira  za  kukatwa  kwa  mshindi  wa kura  za maoni Ludewawanachadema  wakijiandaa kwa maaandamano ya amani  kujiengua na  Chadema  na  kujiunga  ACT  wazalendo

Bango  likimtaka  aliyeteuliwa na chama  kwenda  kugombea  jimbo la Hai kwa MboweAdd caption

Mwanzo  wa maandamano ya  kujiengua na  Chadema

Add caption

wana Chadema katika maandamano  ya  kupinga  uonevu ndani ya  chama

Tuhuma  dhidi ya  Chadema TaifaWanachadema  katika maandamano ya  kupinga mshindi  kutemwaWanachadema  waliojiengua na  kujiunga na ACT  wazalendo  wakiwa nje ya ofisi ya  Chadema  wilaya ya  Ludewa

barua  ya  tuhuma  za  mteuliwa  kutoa  ahadi ya  rushwa hii hapabarua  ikionyeshwa  kwa  wanahabari na  wanachadema

Ni  full jaziba  kwa  wana Chadema  Ludewa

Wanachadema  wakiwa  nje ya  ofisi   ya chama  wilaya  walikokwenda  kurudisha  kadi kabla ya  kuhamia ACT wazalendo

Aliyekuwa mwenyekiti wa BAWACHA  wilaya ya  Ludewa akionyesha  kadi ya  ACT  wazalendo

Aliyeenguliwa Bw  Haule  akiwapongeza wana Chadema kwa kuhamia pamoja  ACT  wazalendo

Wanachadema  wakirudisha  kadi  za chamna  hicho na kujiunga na ACT  wazalendo

Baadhi ya  nguo  na kadi  zikiandaliwa  kuchomwa  moto

katibu wa ACT  wazalendo  Ludewa Alfred Ulaya  akionyesha kadi  za  Chadema 

Wanachadema  wakijipata  kuhamia  ACT wazalendo

Kadi  zikiwa  zimekusanywa kwa kuchomwa  moto

mwana  Chadema  akichoma  moto kadi  za  Chadema Ludewa  kupinga  uonevu  ndani ya  chama  hicho

Add caption

Hivi  ndivyo kadi  zinavyoteketezwa  kwa  moto  baada ya  wana Chadema  kujiengua na  chama  hicho na kujiunga na ACT  wazalendo Mabango  ya  kuagana na Chadema  kwa  wana LudewaBango  likionyesha  Chadema kura  za Chadema  Urais X ,Ubunge X na udiwani X huku  likimaliza kwa  kusema  msituchagulie

Mwanachama wa Chadema  akiongea  kwa jazba  juu ya hali ya mambo ndani ya  Chadema kabla ya  kujiunga na ACT  wazalendo

Ofisi ya  Chadema  wilaya  ikiwa  imefungwa  wakati  wanachadema  walipofika  kurudisha  kadi zaoKadi  ya  ACT  baada ya  kuhama  Chadema

Makada  wapya  wa ACT  kutoka  Chadema 


Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni  akionyesha  barua  nyenye  siri nzito  za  mteuliwa  kununua nafasi hiyo

Bw Haule  akijiandaa  kuchoma moto vifaa vyake vya Chadema kabla ya  kujiunga na ACT wazalendo

…………………………………………………………………………………………..   *Wafanya Maandamano Makubwa. Wachoma Moto
Kadi

* Ofisi 
ya Chadema Wilaya  Nusuru  Ichomwe Moto; 
Viongozi  wakimbia; Watelekeza
ofisi

 Na MatukiodaimaBlog,Ludewa

WANACHAMA zaidi  ya 500 wa 
Chama  Cha  Demokrasia  na
Maendeleo ( Chadema)  Wilayani Ludewa  Mkoani  Njombe
wamekihama  chama  hicho  na kujiunga na  chama 
cha  ACT Wazalendo   wakipinga  hatua ya 
uongozi  wa  juu  wa  chama  hicho kukata 
jina  la  mshindi  wa  kwanza wa  kura  za maoni
Bw. Ocol Haule  na kumteua aliyekuwa mshindi  wa  pili
katika mchakato huo Bw Bartholomeo Mkinga .

Wanachama  hao ambao 
kutoka  kata  mbali mbali  za  wilaya  ya  Ludewa
wamefanya maandamano hayo ya amani leo 
kuelekea   ofisi ya  Chadema  wilaya  huku
wakitishia    kuichoma moto 
ofisi  hiyo  baada ya  viongozi  wake  kuifunga,  kuitelekeza 
na kukimbia kunusuru maisha yao. 

Wakizungumzia  hatua   hiyo ya
kupinga  maamuzi ya  chama ngazi ya 
taifa wanachama hao Bi Hongera  Gama,  Taukile Mapunda  na aliyekuwa 
Mwenyekiti  wa Baraza la  Wanawake 
(BAWACHA) wilaya ya Ludewa Bi. Sophia Mtega  walisema  kuwa wanachama  walikuwa
na  imani  kubwa na mshindi  wa
kura  za maoni  kwani alifanya kazi kubwa ya kukijenga chama
na sio  huyo  waliomuacha katika  kura 
za maoni .

“Kinachoendelea sasa hivi ndani ya CHADEMA ni
ufisadi mtupu,” alisema Bi. Gama akiongeza kuwa yeye binafsi alitoka  CCM na 
kujiunga na Chadema  kutokana
na  mapungufu  yaliyokuwepo  
ndani ya  CCM  ila 
kinachoendelea  kwa  sasa 
ndani  ya  Chadema 
anajuta kuingia Chadema  na  hivyo  ameamua  kuhama chama 
hicho  kumfuata mtu  wao 
waliyemchagua popote atakakokwenda .

“ Mwenendo 
wa  chadema  kwa 
sasa ni  wa  ovyo 
zaidi  kuliko  chama 
chochote  cha siasa hapa nchini
tulikuwa  tukishuhudia  CCM 
watu  wakikatwa ila  leo 
ndani  ya Chadema  imekuwa 
ni kawaida  kuona  wale 
waliochaguliwa na  wanachama
kukatwa na   watu  wachache akiwemo  mwenyekiti 
wa Taifa  wa  chama 
hicho Freeman Mbowe …..tumechoka tunahitaji kwenda  kupata Demokrasia ya  kweli ACT wazalendo sio  ndani ya 
chadema”

Huku Bw Mapunda akidai  kuwa siasa 
za  ukabila  zinaendelea 
kukitesa  Chadema  na 
kuwa  suala   hilo 
la ukabila  na  kuwakumbatia 
mafisadi  ndilo  ambalo 
linaendelea  kukitafuna chama
hicho pia  siasa za  ukanda na 
kukumbatia  ufisadi  imekuwa ni kawaida  Chadema.

Hivyo alisema 
katika kuhakikisha  wana  Chadema 
wilaya ya  Ludewa na   kote 
nchini  wanapinga siasa  za 
ukanda na zile za kuwachukua 
watu  wenye  tuhuma 
za  ufisadi kugombea  ndani ya 
chama  hicho  ni lazima 
wanachadema  kuungana  kupinga hali 
hiyo  kwa  kuhama 
ndani  ya  chama 
hicho na  kujiunga na ACT  wazalendo.

Aliyekuwa 
mwenyekiti wa BAWACHA  wilaya
ya  Ludewa Bi Mtenga  alisema 
kuwa  uonevu  na 
rushwa  vimechangia  wanachama na 
wananchi kukosa  imani kabisa na  chama 
hicho na  sasa badala ya  kuwa chama cha  wanyonge 
kimekuwa ni chama  cha  wenye 
pesa na mafisadi jambo ambalo  wao
kama  wananchi wa chini hawapo  tayari 
tena  kukaa ndani ya  Chadema.

Akimkaribisha 
mgombea ubunge   huyo  aliyekatwa ndani  ya 
Chadema  Bw Haule na  wanachama 
zaidi ya 500 wa  chadema ,
katibu  wa  ACT wazalendo 
wilaya ya  Ludewa Bw Alfred
Ulaya  alisema  kuwa 
pia  alipata  kuwa 
kiongozi  ndani ya  Chadema 
wilaya  ya  Ludewa 
ila alihama  pamoja na  viongozi 
wengine  kutokana na siasa  za chuki ndani ya chama  hicho na hatua ya  kukumbatia 
ufisadi.

Hivyo 
alisema  wanachama  hao 
hawajachelewa  kujiengua na chadema
na kujiunga na chama cha  ACT  wazalendo kwani ni chama chenye  misingi 
bora na chama pekee  chenye
malengo sahihi ya kulikomboa  Taifa  na Chadema na 
pamoja na umoja  wao  wa vyama 
vinavyo unda katiba ya  wananchi
(UKAWA) ni CCM B  hivyo  lazima watanzania  wapenda mabadiliko lazima  kuchagua ACT wazalendo.

Katibu 
huyo  alisema  kwa 
wanachama  wote  ambao 
wamejiengua na Chadema na kujiunga na ACT wazalendo wakiwemo makatibu
na  wenyeviti wa kata   zaidi ya 10 
waliojiunga na ACT wazalendo na viongozi 
wengine  watakuwemo ndani ya  chama 
hicho na vyeo  vyao kama  walivyotoka 
Chadema.

Kwa upande 
wake mgombea  huyo
aliyeenguliwa  kugombea  ubunge 
mbali ya  kushinda kura za maoni
Bw Haule  alisema  kuwa kimsingi aliyeteuliwa  kugombea nafasi hiyo alikuwa amewaandikia
barua baadhi ya  viongozi ngazi ya  wilaya 
ya  kuwaahidi kuwapa  pesa ,kufungua  duka la 
vifaa  mbali mbali pamoja na
kuwahonga  pikipiki barua  ambayo aliinasa na  kuwaonyesha 
wanachama  hao.

Pia 
alisema kimsingi baada ya 
kuenguliwa  kugombea nafasi
hiyo  alitaka  kukaa kimya kama  aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dr  Slaa ila 
akaona  kukaa kimya  bado 
si jibu na  hivyo kuamua  kujiunga na ACT wazalendo na  kuweka 
uozo  huo  wazi.

Bw 
Haule  alisema  kuwa kwa 
sasa atahakikisha anazunguka jimbo nzima 
kufikisha  kilio  chake kwa 
wana Chadema  na  kupinga kwa nguvu  zote wagombea wa udiwani na ubunge wa Chadema
kupewa kura na  kuwa kwa  sasa uhai 
wa Chadema katika  wilaya  hiyo umekufa 
rasmi .

 

NO COMMENTS