Waliokatwa Simba waibukia kwa Mo Dewji

0
361

BAADHI ya wachezaji wa Simba waliotokea kikosi B kabla ya kutemwa katika mazingira ya kutatanisha na kutimkia timu nyingine, wameibuka na kudai kuwa vijana wanaochipukia kwa Wekundu hao wa Msimbazi watafaidi sana kama Mohamed Dewji ‘Mo’ atakabidhiwa timu.

Simba ni moja ya timu zinazosifika kwa kuwa na timu bora za vijana sambamba na Azam FC lakini Wekundu hao wa Msimbazi wanashindwa kuwalea na kujikuta wakiwapeleka timu nyingine bila kupata chochote licha ya kutumia gharama nyingi kuwalea.

Wakizungumza na BINGWA kwa nyakati tofauti huku wakiweka sharti la kutotajwa majina yao, baadhi ya vijana hao walisema wamemsikiliza Mo kwa makini na mipango yake hasa ya kuendeleza timu za vijana na kwamba kama atafanikiwa kupewa timu waliopo watafaidi sana.

“Sisi tumekuwa na bahati mbaya maana tumelelewa pale Simba na tukatarajia tutapata nafasi ya kuitumikia timu yetu lakini cha ajabu tukatemwa kama watoto yatima.
“Tumesikia mipango ya Mo hasa kuhusu timu za vijana, binafsi naamini wale ambao kwa sasa wanachezea timu B wanaweza wakafaidi sana kama mpango wa kumpa mfanyabiashara hiyo timu,” alisema mmoja wa wachezaji hao ambaye aliwika msimu uliopita akiwa na timu nyingine ya Ligi Kuu.

Mwingine alisema: “ Kwanza sisi ambao tulilelewa na Simba kwenye timu ya vijana Simba halafu mwisho wa siku tukajikuta tunaondolewa kienyeji tunaumia sana lakini naamini huu mpango wa Mo utasaidia sana ikizingatiwa ameshaweka wazi juu ya timu za vijana.”

Chanzo: BingwaDSC_1941-640x425

NO COMMENTS