Wachimba madini wa Chile wapokelewa kifalme Marekani

0
373

wachimba madini wa Chile.

Wachimbaji hao 33 wamepokelewa kwa kifahari katika uwanja wa ndege wa Hartfield Jackson huko Atlanta.

Wamealikwa kwa mwaliko maalum wa CNN katika hafla maalum ya kusherekea mashujaa wa CNN (ijulikanayo kama CNN Heroes) inayoadhimishwa usiku wa sherehe za Thanksgiving ambazo ni sherehe kubwa za mavuno na shukrani hapa Marekani na Canada.

Huadhimishwa alhamisi ya nne ya Novemba kila mwaka na si sherehe ya kidini. Wachimbaji hao wamepata mapokezi ya nguvu ikiwa ni pamoja na kusindikizwa na gari la Polisi huko Atlanta.

Wamekuja kwa mwaliko maalum wa CNN ili kushiriki kwenye usiku maalum wa mashujaa wa CNN ambao utaonyeshwa moja kwa moja na CNN Novemba 25,2010.

Wengi wa wachimbaji hao hawajawahi hata kutoka nje ya Chile na wamesafiri kwa mara ya kwanza kutoka nje ya nchi hiyo na kuingia Marekani wameelezea furaha isiyo na kifani.

NO COMMENTS