VILIO, SIMANZI VYATAWALA KUAGWA KWA MTOTO NORAH

0
90

NI huzuni na simanzi kubwa kwa ndugu jamaa na marafiki iliyoambatana na vilio wakati wa shughuli yaa kuaga mwili wa mtoto Norah Jimmy (11) aliyefariki dunia juzi kwa kile kinachodaiwa kuwa alibakwa kisha kunyongwa.
Norah aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Atlas iliyopo Sinza, ameagwa Jumanne nyumbani kwao maeneo ya Sinza Mori jijini Dar na anatarajiwa kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni.


Inadaiwa mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili cha kubakwa kisha kunyongwa mpaka kufa na mjomba wake aitwaye John Msigala.

Mpaka sasa bado haijatolewa ripoti ya daktari ya kuthibitisha chanzo cha kifo cha Norah,  huku jeshi la polisi likisisitiza waombolezaji wa msiba huo kuvuta subira mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.
Chanzo:Global publishers.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY