VIJANA 1000 WAKUTANA WASHINGTON DC KATIKA MANDELA WASHINGTON FELLOWSHIP.

0
99

Vijana wapatao 1000 walishirikia katika mafunzo ya wiki sita nchini Marekani katika vyuo mbali mbali ikiwa ni mpango ulioanzishwa na rais Obama ujulikanao kama Mandela Washington Fellow, baada ya kukamilisha masomo yao vijana hawa wamekamilisha kwa mkutano wa siku siku 4 uliofanyika katika hoteli ya Marriot Marquiz mjini Washington Dc.
Vijana hawa wametoka katika nchi 49 barani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na wamepitia usaili wa hali ya juu kwa jumla waliopeleka maombi walikuwa vijana wapatao 60,000 lakini waliopata nafasi ni vijana 1000 tu.
Ili kijana aweze kupata nafasi hiyo inabidi aonyeshe kazi zake ambazo si za kumasaidia yeye tu bali pia jamii iliyomzunguka , kwa hiyovijana waliokuja hapa ni pamoja na madaktari bingwa katika magonjwa mbali mbali, wauguzi, wajasiriamali, wanaharakati mbali mbali wa haki za kijamii, wanwake , watoto n.k.
Pia vijana hawa wameweza kujipatia mambo mengi ambayo watarudisha nyumbani Afrika mmojawapo ni daktari bingwa wa kansa kutoka Tanzania Heri Tungaraza ambaye alipata nafasi kujifunza kutoka katika hospitali zinazoongoza katika matibabu ya kansa nchini Marekani huko Emory University na Cancers Centers of Amerika waliko madaktari bingwa wa kansa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya kansa Heri Tungaraza wa Tanzania.

Daktari huyu anasema amepata mbinu za madaktari wa Mrekani ambao wanafanya kazi kwa kushauriana kama timu , si mpaka mmoja ashindwe ndio atafute mwenzie wasaidiane mawazo anasisitiza atalipeleka hilo kwenye kliniki na hospitali za nchi yake Tanzania ili madaktari wafanya kazi kama timu kwani kuunganisha kichwa zaidi ya kimoja ni kitu kizuri na madaktari wapeane mawazo matokeo yake kuti kama timu ni kitu kizuri.

Vijana hawa wameweza kufanikiwa pia kushirikiana uzoefu wa yale mbali mbali wanayofanya katika nchi zao kwa mfano Whinnie Singwa alikulia akiwa yatima alipoteza wazazi wake akiwa na umri wa miaka 6 na alipelekwa kulelewa na shangazi yake , ambaye kwa bahati mbaya yule shangazi mwingine alifiwa na mume kwa hiyo akajikuta anaangukia mitaani akiwa na umri wa miaka 8 anasema alilala kila mahali na alisumbuliwa sana na wanaume, makondata wa matatu, waendesha piki piki na wasio na ajira, akajikuta anaanza kuvuta sigara na mambo mengine.

Lakini kijana huyu maisha yake yalibadilika baada ya kuchukuliwa na Compassion International ambao walimchukua akiwa na umri wa miaka 10 na kumrudisha shule na kumpa malezi hatimaye alisoma sekondari mpaka chuo kikuu na kuchukua masomo ya Sosholojia.

Sasa ameamua kurudi na kusaida jamii yake akisaidia wasichana wapatao 500 katika kituo chao baada ya kupitia yote hayo sasa anawasaidia watoto yatima na wasio na makazi nchini Kenya.
VOA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY