Utata Waibuka Kuhusu Alipo Mchora Katuni Masoud Kipanya

0
120

Majira ya jioni leo Januari Mosi 2018 zimesambaa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kwamba, mchora katuni maarufu Tanzania, Masoud Kipanya amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi.

Taarifa hizo zinadai kuwa, Masoud Kipanya ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds FM, amekamatwa na Polisi baada ya kuchora katuni ambayo ina maudhi ya uchochezi kati ya wananchi na serikali.

Baada ya kuibuka kwa utata huo, mwajiri wa Masoud Kipanya, Clouds Media Group (CMG), imeeleza kuwa, kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi kufahamu alipo mtangazaji huyo.

“Uongozi wa Clouds Media Group (CMG) unawaomba wananchi wote nafasi ya utulivu wakati tukiendelea kuzifanyia kazi taarifa kamili wapi alipo Masoud Kipanya. Uongozi utaoa majibu ya kina.”Kusoma zaidi bofya

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam bado halijatoa taarifa kama linamshikilia mtangazaji huyo ama la.

Masoud amekuwa akichora katuni zinazoelezea masuala mbalimbali yanayoigusa jamii kuanzia kwenye uchumi, siasa, masuala ya kijamii na pia kitamaduni.

UPDATES:

Masoud Kipanya amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi baada ya kuchora katuni inayochonganisha serikali na wananchi. Haijaelezwa amepelekwa kituo kipi cha polisi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY