Ujumbe wa Wazi wa Eric Shigongo kwa Diamond Platinumz Wazua Gumzo Mitandaoni

0
227

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Mhamasishaji na Mwandishi wa Vitabu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo amemwandikia ujumbe wa wazi mkali wa Afro Pop Barani Afrika, Diamond Platinumz umezua gumzo mitandaoni ambapo kila shabiki amekua akitoa maoni.
Katika ujumbe huo ambao Shigongo aliandika jana Machi 28 na kueleza kuwa ataendelea tena kuandika sehemu ya pili leo Machi, 29 kupitia Instagram yake, Shigongo ameandika hivi.
========
“MY CONFESSION

Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo.
Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania.
Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO!
LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake.
Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE.
Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.
Nitaendelea kesho” (yaani leo Machi 29, 2017).
GPL

NO COMMENTS