UCHAGUZI ANGOLA MACHO NA MASIKIO KWENYE MAFUTA NA MTOTO WA DOS SANTOS

0
255

Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola .
Angola inajiandaa kwa uchaguzi wa kihistoria ambao kiongozi wake wa muda mrefu Jose Eduardo Dos Santos ataachia madaraka baada ya miaka 38 lakini wakati taifa hilo linajiandaa kupiga kura wachambuzi ndani na nje ya nchi hiyo wanasema wanaangalia kwa ukaribu si sanduku la kura bali kwenye mahesabu ya biashara ya shirika la mafuta la serikali nchini humo Sonangol.
Uchaguzi wa Agosti uko wazi ni kati ya chama tawala na upinzani uliojiimarisha . Mshindi atasimamia taifa ambalo uchumi wake kwa kiasi kikubwa unategemea uzalishaji mafuta ambao ni kiasi cha asilimia 45 ya pato la taifa na asilimia 95 ya bidhaa zinazosafirishwa nje .
Wakati Dos Santos anajiandaa kuondoka madarakani wengi wanajiuliza shirika hilo litakuwaje ambalo kwa sasa linaendeshwa na mwanamke tajiri kuliko wote Afrika ambaye ni mtoto wa rais.
Isabel Dos Santos na familia yake wamekwepa shutuma nyingi za kujirudia za rushwa iliyokithiri.

VOASWAHILI.COM

NO COMMENTS