UBINGWA WANUKIA MSIMBAZI BAADA YA SIMBA KUIBWAGA YANGA

0
602

Mchezo wa Simba na Yanga Jumamosi ulikuwa ni muhimu kwa timu zote mbili kwa sababu timu zote ziko kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu.

Simba iko njia moja ikiwa bado inaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 23 huku Yanga wakisaliwa na pointi zao 49 pointi tano nyuma ya Simba lakini Yanga wanamchezo mmoja mkononi wakiwa wamecheza mechi 22.

Katika mchezo wa Jumamosi Yanga walianza kupata goli dakika ya tano ya mchezo kwa mkwaju wa penati baada ya Novalty Lufunga kumwangusha mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa kwenye eneo la hatari wakati akielekea kufunga.

Simon Msuva akakwamisha kambani mkwaju huo kwa kupiga mpira upande wa kushoto wa golikipa Daniel Agyei lakini ukiwa ni upande wa kulia wa Msuva.Kusoma zaidi bofya

Baada Simba kuruhusu goli, kocha wa Simba Joseph Omog alifanya mabadiliko kwa kumtoa Juma Liuzio na kumuingiza Said Ndemla ambaye kwa kiasi kikubwa akaituliaza timu kwenye nafasi ya kiungo wa kushambulia.

Kipindi cha kwanza kikamalizika Simba wakiwa nyuma kwa goli moja huku Yanga wakiwa mbele kwa goli moja la Simon Msuva.

Kipindi cha pili wakati Simba ikiwa inapambana kupata goli la kusawazisha, ikpata pigo baada ya beki wao wa kulia Javier Bokungu kuondolewa uwanjani kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Obrey Chirwa nje kidogo ya eneo la box.

Kocha wa Simba akafanya tena mabadiliko kwa kumuingiza Shiza kichuya kuchukua nafasi ya Mohamed Ibrahim ‘MO’.

Kadi nyekundu ya Bokungu ikalazimisha benchi la ufundi la Simba kufanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Novalty Lufunga kisha akaingia Jonas Mkude ambaye alienda kucheza nafasi ya kiungo wa ulinzi aliyokuwa ikichezwa na James Kotei ambaye alirudi kucheza katika beki ya kati sambamba na Abdi Banda.

Simba wakapata bao la kwanza na la kusawazisha dakika ya 66 lililofungwa na Laudit Mavugo kwa kichwa aliyeunganisha pasi ya Kichuya kutoka upande wa Kaskazini Mashariki ya uwanja.

Kichuya akapeleka ushindi Msimbazi baada ya kufunga bao la pili huku likiwa ni goli lake la 10 msimu huu katika ligi kuu Tanzania bara.
Kwa hisani ya Shafih Dauda.

NO COMMENTS