Trump atoa njia mbadala za kuilazimisha Mexico kulipia ukuta

0
282

Ikulu ya White House imesema kuwa Rais Donald Trump ana “njia mbadala” za kuilazimisha Mexico kulipia gharama za ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico.

Mipango ya ukuta huu wenye utata tayari umeharibu mahusiano ya Mexico na Marekani, baada ya siku chache Trump kuchukua madaraka.

Mapema Alhamisi, msemaji wa ikulu ya White House Sean Spicer amewaambia waandishi kuwa Trump ametaka Mexico ilipe kodi ya asilimia 20 ya bidhaa wanazoingiza nchini.

Mexico kulipishwa kodi mpya

Alisema kodi hii mpya itaiingizia Marekani $ bilioni 10 kwa mwaka “itayoweza kulipia gharama ya ukuta.” Amesema pia Rais Trump amelijadili suala hili na viongozi wa Bunge na ametaka uamuzi huu uwepo katika mpango wa kina wa marekebisho ya kodi ambayo Bunge itabidi kuupitisha.

Lakini baadae, Ikulu ya White House imesema wazo hilo ni moja kati ya njia mbadala zilizoko mbele yake za kugharimia ukuta huo kusini mwa mpaka huo.

Na imesema Trump anatarajiwa kufanya uamuzi juu ya namna ambayo Marekani itarudisha gharama za pendekezo lake la ujenzi wa ukuta huo.

Walipa kodi wa Marekani mwanzoni watagharimia ukuta huo, ambao unategemea kutumia mpaka $ milioni 15.

Umuhimu wa biashara na Marekani

Hata hivyo haijulikani ni hatua zipi Mexico ingeweza kuchukua iwapo ushuru wa mpakani utapitishwa, kwa sababu bidhaa zao wanazosafirisha Marekani ni muhimu kwa uchumi wake.
VOA

NO COMMENTS