TRUMP ASIFU UONGOZI WA SADDAM NA KULAANI WAANDISHI

0
467

Ni karibu miaka kumi sasa tangu kiongozi wa Iraq, Saddam Hussein, alipouwawa baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Jumanne, Hussein lilikuwa jina lililovuma sana kwenye mtandao wa Twitter baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Repablikan hapa Marekani, Donald Trump, kusifu uongozi wa Saddam Hussein.

Trump ameshawahi kutoa matamshi sawa na hayo hasa 2014 alipoandika kwenye Twitter kwamba Iraq sasa ni hatari kuliko ilivyokuwa wakati wa uongozi wa Saddam Hussein.

Trump amesema kuwa aliekuwa Rais wa Marekani, George Bush, pamoja na Rais Barack Obama wanahitaji kuomba msamaha kwa kuamuru vita vya Iraq.

Lakini jumatano latika hotiuba yake Cincinati Ohio alimlaumu mwandishi Chuck Todd wa Meet The Press kwa kutosema ukweli kwamba yeye alichosema ni kwamba Saddam alikuwa mtu mbaya ila aliuwa magaidi.

Aliwaita CNN-Clinton News Network akidai wanamuongelea mno mpinzani wake huyo na kumsema yeye vibaya.
VOASWAHILI

NO COMMENTS