Trump ashinda kiti cha urais Marekani.

0
518

trump-2Donald Trump ameweka historia ya kuwa mgombea wa kwanza asiye mwanasiasa kushinda uchaguzi wa Marekani jambo ambalo wachambuzi wengi walikuwa wakisema ni gumu kufanyika.

Trump alijihakikishia ushindi baada ya kunyakua majimbo muhimu ya Florida, North Carolina na Ohio ambayo yalikuwa yenye ushindani mkubwa na ambayo hakutarajiwa kushinda yote kwa pamoja.

Ukumbi wa Javits Center Ny ulibaki kimya baada ya Trump kutangazwa kuchukua ushindi wa jimbo la Florida, kitu ambacho kilionyesha wazi kukatishwa tamaa kwa wafuasi wa Clinton.
Mapema usiku wa Jumanne mwenyekiti wa kampeni ya Clinton, John Podesta aliwataka mamia ya mashabiki walokusanyika katika ukumbi mjini New York kurudi nyumbani na kwamba mgombea wao hatazungumza.

Muda mfupi baadae mgombea mwenza wa chama wa Trump Mike Pence amewashukuru wafuasi na kumkaribisha rais mteule wa 45 wa marekani. Hii ikiwa ni tukio la kihistoria Marekani kwa mtu ambae hajawahi kushika nafasi au wadhifa wowote wa serikali kuchaguliwa kuliongoza taifa kuu la dunia.

Trump akiwahutubia wafuasi hao huko New York amesema Hillary amempigia simu na kumpongeza. Mfanyabiashara huyo ametoa wito kwas wamarekani wa pande zote kuungana na kufanya kazi pamoja.

Trump itakumbukwa alianza kampeni yake kwa kutoa maneno makali dhidi ya uhamiaji haramu na kujenga ukuta hiyo ni kampeni ambayo imeungwa mkono na wengi weupe ambao si wasomi na hakujulikana kama ingeweza kutokea.

Trump kwa kiasi fulani wachambuzi wanaeleza ameshinda si kwa kampeni ya kawaida na alitumia sana mitandao na umaarufu wake wa TV kuweza kushinda uchaguzi huu jambo ambalo wengi hawakuliona .

NO COMMENTS