Trump akataa waliobadili jinsia kuajiriwa katika jeshi la Marekani

0
80
Republican presidential candidate Donald Trump speaks to supporters as he takes the stage for a campaign event in Dallas, Monday, Sept. 14, 2015. (AP Photo/LM Otero)

Rais wa Marekani, Donald Trump Jumatano amesema watu waliojibadili jinsia
hawatakubaliwa kujiunga na jeshi hilo tena kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Mwezi uliopita, Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis alichelewesha
kuidhinishwa kwa mpango huo wa rais Obama wa watu waliobadili jinsia kujiunga na
jeshi la Marekani.
Inakadiriwa kuwa jeshi hilo linao watu waliobadili jinsia wapatao 4000.

“Baada ya kushauriana na wajumbe wangu na wataalamu wa kijeshi, tumeshauriwa kuwa Serikali ya Marekani haitakubali au kuruhusu watu wasio na uwezo wa kutumikia kwa uwezo wowote katika Jeshi la Marekani,” Trump alitweet .
“Jeshi letu linapaswa kuzingatia ushindi mkubwa na ushindi na hauwezi kulemewa na gharama kubwa za matibabu kwa kuwaingiza jeshini au kuwakubali watu waliobadili jinsia zao,” Trump aliongeza.
Source:VOA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY