TP Mazembe yatinga fainali klabu bingwa ya dunia

0
567

Mulota wa Tout Puissant Mazembe akishandilia bao la kwanza
Timu ya TP Mazembe hatimaye imeweka historia ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kuingia fainali ya vilabu duniani ya FIFA. TP Mazembe imeingia fainali hizo baada ya kuwabwaga kwa mshangao mkubwa mabingwa wa Brazil na miamba ya soka duniani Internacional kwa 2-0.

Walikuwa ni Mulota Kubangu na Dioko Kaluyituka waliopeleka kilio Brazil baada ya kuweka kimiani mabao safi kunako dakika za 53 na 85. Ni furaha iliyoje kwa mabingwa hawa wa Afrika na bara zima kwa hatua hii kubwa waliyofikia Tp Mazembe.

Sasa “Tout Puissant Mazembe” iko katika nafasi nzuri kabisa ya kunyakua kombe hilo baada ya kuwang’oa vigogo hawa wa Brazil, kwa hiyo sasa watakwaana na mshindi kati ya FC Internazionale Milano maarufu kama Inter ya Italia na Seongnam Ilhwa ya Korea Kusini wanaocheza nusu fainali ya pili Jumatano.

Wachambuzi wa soka wanasema huu ndio utakuwa mtihani wa kumjenga au kumwondoa kocha wa sasa wa Inter Rafael Benitez kwenye huo mchezo mkali dhidi ya vijana wa Korea Kusini.

Kocha huyo amedai wana uwezo wa kushinda hasa baada ya kurudi kwa mshambuliaji wake Diego Milito kazi itajulikana baaada ya dakika 90.

NO COMMENTS