Kila la kheri timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”

0
496

Timu ya taifa ta Tanzania Taifa Stars imekataa kuwa kichwa cha mwendawazimu kwa kutoka sare ugenini na timu ya Taifa ya Algeria “Desert Foxes”  kwa bao 1-1  kitendo ambacho ni cha kishujaa. Hii ni katika michuano ya kutafuta nafasi ya kucheza kombe la mataifa ya Afrika 2012 huko equatorial Guinea na Gabon . Je safari hii wakiwa na kocha mpya timu hii itaweza kuwatoa watanzania kimaso maso? Mechi zilizopo mbele yao ni dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati na  Morroco ambapo ni katika kundi D.

Tanzania inahitaji kushinda mechi tu 3 ambazo watacheza nyumbani ili waweze kuondoa ukame wa miaka 30 kutoshiriki kombe la mataifa ya Afrika . Na si hivyo kundi hilo ambalo awali nafasi walipewa Morocco na Algeria liko wazi kwa yeyote baada ya Morroco kushikiliwa koo na Afrika ya kati na kutoka sare 0-0.

Mechi ijayo ya Tanzania itakuwa nyumbani dhidi yaMorroco “Simba wa Atlas”  na hii ndio nafasi yao ya kufanya kweli na kujipatia ushindi nyumbani hapo Novemba 9. Tanzania hivi sasa iko chini ya kocha mpya Jan Poulsen kutoka Denmark ambaye alikuwa mmoja wa mafundi  katika kikosi kilichochukua kombe la Ulaya 1992. Anategemewa kufanya mabadiliko ambayo tayari yanaanza kuonekana lakini wasibweteke kazi wanayo kubwa mbele yao.

Kila la kheri Taifa Stars!

NO COMMENTS