TID afunguka sababu ya kufanya ziara yake Burundi.

0
366

Hivi karibuni zimeweza kusambaa picha kadhaa mitandaoni zikimuonyesha muimbaji huyo akiwa nchini humo akifanya show na nyingine zikimuonyesha akiwa na Christian Bella.

Akiongea katika kipindi cha Dj Show cha Radio One, TID amesema, “Kikubwa zaidi ilikuwa ni kuja kufanya TV and Radio promotion tour. Nimekwenda radio kadhaa na TV kadhaa, hii ilikuwa kutambulisha wimbo wangu mpya ‘Woman’ na ile niliyomshirikisha Tofy ni msanii wa huku lakini anaishi South Africa. Nikaenda mkoa unaitwa Rumonge ni kama masaa mawili kwa kuendesha ukitoka Bujumburani nikaimba hapo na concert ilijaza sana. Na siku inayofuata nikaenda Nagara kufanya concert nayo ilijaza tena vile vile.

“Experience ambayo nimeipata kutokana na tour hii, nimegundua love ipo kubwa sana kutoka kwa mashabiki kwa ujumla wa TID, mashabiki wa Bongo Flava watu wanathamini sana Bongo Flava especially waasisi au wakongwe,” ameongeza.

Msanii huyo ameongeza kuwa tayari amepata dili la kurudi tena kutumbuiza nchini humo baada ya mwezi wa mtukufu wa Ramadhan.
Bongo5.com

NO COMMENTS