TANZIA: MKE WA MZEE KINGUNGE AFARIKI DUNIA

0
101

MKE wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kueleza kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.
“Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling’atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka,” amesema.
Chanzo:Global publishers

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY