Taasisi ya kupambana na rushwa Tanzania yaahidi mapambano wakati wa uchaguzi

0
461

Ikiwa vugu vugu la uchaguzi Tanzania linazidi kupamba moto taasisi ya kupambana na rushwa (TAKUKURU)  nchini humo imedai itawasweka ndani na kuwafungulia mashitaka wale wote ambao watajihusisha na rushwa.

Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa amedai kuwa sheria zimewekwa mwaka huu kwa mara ya kwanza na kusema watakaobainika watachukuliwa hatua  ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kushiriki katika uchaguzi.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) msajili huyu amesema wagombea wanaweza kutoa misaada kupitia vyama vyao pekee  na sio moja kwa moja kwa wapiga kura.

Lakini swali ambalo wachambuzi wengi wanajiuliza haya ni maneno tu au kutakuwa na utekelezaji wa aina fulani? mwanasheria na mtalaam wa masuala ya katiba  Bw.Alex Mgongolo akizungumza na sauti ya Amerika amesema wananchi wengi bado hawafahamu sheria za rushwa na hili linaweza kuwa tatizo maana kwa maana rushwa inaathiri mtoa rushwa na mpokeaji.

Hivi karibuni taasisi ya Transparency International imetoa orodha yake ya nchi zenye rushwa iliyokithiri Afrika Mashariki ambapo namba moja ilikuwa Burundi ikifuatiwa na Uganda ya tatu ikiwa Kenya na ya nne Tanzania.

NO COMMENTS