Tanzania yaadhimisha siku ya Uhuru kwa kufanya usafi.

0
756

8Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Janeth Magufuli akiongoza kufanya usafi katika viunga vya Ikulu Daresalaam.

Tanzania leo inaadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo baadaye iliungana na Zanzibar kufanya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambapo rais wa nchi hiyo John Magufuli ameongoza raia wa kufanya shughuli za usafi nchi nzima.
Rais huyo alishiriki kwenye zoezi hilo la usafi katika maeneo ya kuzunguka Ikulu mjini dar es salaam hadi kwenye soko la samaki la feri, na kueleza kuwa ni aibu kwa Taifa kukumbwa na kipindu pindu kwa sababu ya uchafu.
Miaka yote Tanzania imekuwa ikiadhimisha sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika kwa Gwaride maalum la kijeshi lakini Rais Magufuli ambaye aliingia madarakani baada ya uchaguzi wa oktoba aliamua watanzania washerehekee kwa kufanya usafi ili kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa kipindu pindu.
www.voaswahili.com

NO COMMENTS