Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Boehner ajiuzulu

0
447

17D2B409-A04B-43CC-B796-221A5DE96914_w640_r1_sJohn Bohner spika wa Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani ametangaza atajiuzulu kutoka bunge mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, tangazo ambalo limewashtusha wanasiasa na wananchi kwa ujumla.

Boehner, mbunge tangu 1990 amekuwa akikabiliwa na kishinikizo kutoka tawi la wenye siasa kali katika chama chake cha kihafidhina cha Republican kuhusu masuala kadhaa ya kisiasa na kijamii.

Nyadhifa ya spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani ni nafasi ya pili katika kuchukua uwongozi wa serikali ikiwa wote rais na makamu rais wanashindwa kuendelea na kazi zao.
Papa Francis akiwapungia mkono watu kutoka afisi ya Spika BohnerPapa Francis akiwapungia mkono watu kutoka afisi ya Spika Bohner

Tangazo la Boehner limetolewa siku moja baada ya kumkaribisha Papa Francis kulihutubia bunge, ambapo alitoa wito kwa wabunge wote kuacha mivutano na kutekeleza kazi walopewa na wapiga kura.

Boehner alichaguliwa na wabunge wenzake wa Republican kuwa spika karibu miaka mitano iliyopita na alijaribu kujiuzulu mwaka 2014 lakini kutokana na kushindwa kwa naibu wake Eric Cantor katika uchaguzi wa bunge aliamua kuendelea kubaki.

Akizungumza kutokana na tangazo hilo spika aliyemtangulia Mdemocrat Nancy Pelosi amesema uwamuzi huo unaonesha jinsi kuna mvutano mkubwa ndani ya chama cha Repuclican kutokana na masuala mbali mbali yenye maslahi kwa wananchi.
Chanzo:voaswahili.com

NO COMMENTS