Siogopi kufungwa – Rais Magufuli

0
65

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema atawatetea Watanzania kwa nguvu zake zote juu ya majizi huku akisema haogopi kufungwa badala yake majizi ndio yatakayo fungwa.

Rais Mgufuli amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika Uwanja wa Lake Tanganyika ambapo amehutubia wananchi.
“Siogopi kufungwa. Kama mliniteua niwatetee, nitawatetea kwa nguvu zangu zote juu ya majizi, tumeibiwa vya kutosha, madini yetu yanachimbwa yanapelekwa nje na hatupati kitu,” amesema Rais Magufuli.
“Wengine wamelipwa pesa ili kupinga tusichukue hatua dhidi ya majizi, nawaambia mimi kama rais nimejitoa kufa na kupona mpaka nihakikishe mali za Watanzania wanyonge haziibiwi na haki yao wanaipata.Watambue kwamba sitafungwa badala yao majizi ndiyo yatafungwa. Ilikuwa lazima tubadilishe sheria zetu hatuwezi kuendelea kuibiwa rasilimali zetu.”
Source:Bongo5.com

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY