Simon Msuva ameanza kwa kufunga Morocco game ya kwanza

0
159

Winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Simon Msuva aliyekuwa anaichezea Yanga, Jumapili ya July 30 ikiwa ni siku nne zimepita toka asaini mkataba na timu ya Difaa El Jadid ya Morocco, ambapo ni mafanikio kutoka kucheza Tanzania nchi iliyopo nafasi ya 114 katika viwango vya FIFA anakwenda kucheza nchi iliyopo nafasi ya 60.
July 30 amepata nafasi ya kuichezea timu yake ya Jadid mchezo wa kwanza wa kirafiki na kufunga goli wakipoteza kwa magoli 2-1, kocha wa Jadid aliamua kuchezesha vikosi viwili katika mchezo huo ambapo kila kikosi kilicheza kwa dakika 45.
Dakika 45 za kwanza kocha wa El Jadid alichezesha wachezaji aliyopandisha kutoka team B na wachezaji wanaofanya majaribio ambapo kikosi hicho kilifungwa magoli mawili na ndio dakika 45 za pili Simon Msuva na wachezaji wengine wakaingia na Msuva akafunga goli la kufutia machozi.
Source:Millardayo

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY