Shule ya Southern High lands Mafinga yazidi kupaa.

0
737

 Wanafunzi  wa shule ya  Southern Highlands Mafinga wakiwa katika mahafali  yao  ya  14  Mwaka jana

Na MatukiodaimaBlog
MKURUNGENZI 
mtendaji  wa  shule ya  Southern 
Highlands Mafinga  mkoani Iringa Bi Mary  Mungai amewapongeza walimu 
na  wafanyakazi  wa  shule hiyo kwa kuiwezesha  shule   hiyo  kuendeleza
rekodi  yake ya  kufanya vizuri katika matokeo  ya  mtihani  wa Darasa
la Saba  kiwilaya  ,kimkoa na hata  Taifa  kwa  miaka zaidi ya 13  sasa.

Bi 
Mungai  alitoa pongezi hizo  kwa  walimu   wakati akielezea mafanikio 
ya  shule   hiyo leo   kuwa kwa  mwaka  huu shule   hiyo  imeweza 
kuongoza  tena  kiwilaya  kwa kushika nafasi ya  kwanza  kati ya shule
171 zilizopo wilayani Mufindi na shule  ya  7 kati ya shule 467 katika 
mkoa  wa  Iringa na  kitaifa kuwa  shule ya 888 kati ya  shule 16,096

Hata 
hivyo  alisema  kuwa  kwa mwaka  jana  shule  hiyo  ya  Southern
Highlands Mafinga  ilikuwa nafasi ya  kwanza  kiwillaya kati ya  shule
167 na  kimkoa  ilikuwa ya 8  kati ya shule 458 na  kitaifa  ilikuwa 
nafasi ya 353 kati ya  shule 15,867  kuwa matokeo  ya mwaka  huu
yameonyesha  ni kwa  kiasi gani  jinsi walimu  wa  shule   hiyo 
walivyoendelea kujituma  zaidi katika  ufundishaji .


Alisema  kuwa matokeo hayo ya darasa la 
saba  katika  shule   hiyo yanaonyesha ni kwa  kiasi gani walimu 
wanavyoendelea kuifanya  shuler hiyo kutoa elimu   ubora   na  sio 
bora  elimu hivyo kuwafanya   wazazi  waliowengi kuendelea kuchagua 
shule  hiyo
kwa  ajili ya  kuwapatia   elimu  bora.

Mkurugenzi 
huyo alisema siri  kubwa  ya  walimu  kufanya kazi vizuri  inatokana
na  ubunifu  wa safu ya  uongozi  wa  juu  wa  shule hiyo kwa  kuwapa
motisha  walimu kila  mwaka pindi wanapofanya vizuri katika  mitihani
na  kwa  wanafunzi pia  wamekuwa  wakipongezwa toka wanapoanza darasa
la  awali hadi wanapomaliza pindi  wanapofanya vizuri  katika  mitihani 
yao.


Alisema  kuwa  shule  ilianzishwa  mwaka 1994 kama
chekechea  kwa  jina  la  Lusungu Day Care Center ,Mwaka  1997 ilikuwa
na  kuanza shule  ya  msingi  -primary  school ndiyo sasa  inaitwa 
southern Highlands yenye  usajili  wake  namba IR03/7/001 ya  mwaka 1997
ambapo  imekuwa  ni  shule  ya pili kufunguliwa  baada ya  Brook Bond“ Uongozi  wa  shule  umekuwa ukihakikisha  unakuwa na 
mpango endelevu  wa  kuboresha mazingira  ya  shule pamoja na 
kuboresha  elimu  zaidi ili  shule  hiyo  kuendelea  kubaki  ya mfano 
katika taalum mkoa  wa  Iringa na nje ya  mkoa wa Iringa”

Aidha alisema  kuwa mbalia  ya  wanafunzi 
wa  shule hiyo kuwa na utaratibu wa kufundishwa masomo mbali mbali 
darasani ila  bado  shule  imekuwa na utaratibu  wa  kuwapeleka  
wanafunzi katika mafunzo maeneo mbali mbali yakiwemo  ya  vivutio vya
utalii katika Tanzania  bara na  visiwani  lengo  likiwa ni  kukuza
uelewa  zaidi wa  watoto  hao.

Bi Mungai alisema  kuwa  mbali
ya kutembelea  maeneo mbali mbali ya  nje ya mkoa  pia  shule  imekuwa
na utaratibu  wa  kuwapeleka  kujifunza  pia katika mashirika  yaliyomo
ndani ya mkoa wa Iringa na Njombe .

alisema 

ushirikiano mzuri  ambao  wazazi  wamekuwa  wakionyesha  katika  shule 
hiyo  hivi  sasa tayari  shule   hiyo imeanzisha   shule ya 
sekondari   ambayo  inawawezesha  wanafunzi hao  kuendelea  na  elimu 
ya  sekondari na kama  njia ya  kuondoa  usumbufu  wa  wanafunzi  kukosa
nafasi  za  sekondari pindi  wanapofaulu .


Kwa  upande  wake kaimu  afisa
 elimu  wa  Nasibu A. Mengele  alisema  kuwa  kati ya  shule ambazo
 zimekuwa  zikiupatia  sifa  mkoa  wa Iringa kwa kufanya vizuri katika
mitihani ya darasa la  saba ni pamoja na shule  hiyo ya Southern
Highlands Mafinga   hivyo wao kama  viongozi wa elimu  wataendelea
kuitolea  mfano shule  hiyo kila sehemu na ikiwezekano kuitangaza  zaidi
 ili  wazazi  kusomesha  watoto  wao katika  shule hiyo.

Mwalimu 
mkuu  wa shule  hiyo Bw Joson Nyang’wara alisema  kuwa jumla  ya 
wanafunzi 51  ndio  waliofanya mtihani  wa  darasa  la  saba  na 
wanafunzi  wote  wamefaulu katika mtihani  huo hivyo  alisema   kuwa
suala la  wanafunzi hao  kukosa nafasi halipo kwani tayari shule   hiyo
ya Southern Highlands Mafinga imekwisha kamilisha shule  yake ya 
sekondari ambayo  imeanza   kazi toka mwaka jana.

NO COMMENTS