SHUKURANI ZA DHATI.

0
533

IMG_3203Familia ya Mikidadi DMV na Tanzania inapenda kutoa shukurani za dhati kwa wale wote kwa nia moja au nyingine waliungana na familia ya Mikidadi kwa hali na mali Tanzania na Marekani na kuwafariki katika kipindi hiki kigumu kwao cha kuondokewa na mpendwa baba yao Mzee Mikidadi aliyefariki siku ya Jumamosi March 21, 2015 na kuzikwa siku ya Jumapili March 22, 2015 katika makaburi ya Magomeni Mtambani.

Familia inependa kutoa shukurani zake kwa marafiki wa Ally Mussa Mikidadi na Watanzania wa Marekani pamoja na kwamba Marekani ni nchi ya mchaka mchaka, mmeacha shughuli zenu na kujumuika pamoja na mfiwa na kumfariji kwa wengine kupiga simu, kufika nyumbani kwa mfiwa na huku wengine wakisafiri toka majimbo mengine na kikubwa zaidi siku ya kisomo Ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wa Marekani mmechukua muda wenu kuandaa chakula na vinywaji kwa ajili ya kufanikisha kisomo cha mpendwa baba yetu. Kusema ukweli hatuna tutakalo walipa litakalo lingana na yote mliomfanyia Ally Mussa na familia ya Mikidadi.

Mwisho bila kuwasahau Watanzania na marafiki wa Ally Mussa ambao wapo Tanzania kwa kuacha shughuli zao na kufika nyumbani Magomeni Mapipa na kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mzee Mikidadi yote hayo hatuna zaidi ya kusema asante japo asante hailingani hata chembe na yote makubwa mlioifanyia familia hii, tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awalipe na awazidishie zaidi.

Kama kuna yeyote tutakua tumemsahau tunaomba radhi na ajue sio kusudio letu

Asante sana kwa wema na ukarimu wenu.

NO COMMENTS