Shambulizi la bomu Kenya watu 3 wapoteza maisha

0
317

Polisi nchini Kenya wamesema bomu lililokuwa ndani ya gari lilipuka pembeni ya basi huko Nairobi na kuuwa watu wapatao watatu na kujeruhi wengine 26.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) Maafisa wanasema bomu hilo lilipuka wakati abiria wakijitayarisha kupanda basi ambalo lilikuwa linatarajiwa kwenda Kampala Uganda.

Polisi wanasema abiria aliokuwa amebeba begi hilo lenye mabomu alipogundua mapolisi wanapekuwa mizigo yote alitupa begi hilo na kujaribu kukimbia.

Hata hivyo ni mmoja wa waliofariki dunia.

Wakati huo huo mkuu wa Polisi wa Uganda alishatoa onyo juu ya uwezekano wa vitisho vya kigaidi kutoka kwa alqaida na makundi mengine ya kiislam yenye msimamo mkali ikiwa ni pamoja na Al Shabab ya Somalia wakati wa sherehe za Krismas.

NO COMMENTS