Serikali yazindua mkakati kukabiliana na ajali, haya ni mambo 14 yaliyolengwa

0
396

Baraza la Taifa la usalama barabarani Tanzania limeibuka na mkakati wa miezi sita unaolenga kukabiliana na ajali za barabarani nchini kwa muda mfupi kuanzia mwezi huu mpaka February 2017. Katika mkakati huo uliozinduliwa leo umelenga katika kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwa ambayo hupelekea ajali za barabarani kuongezeka, mambo yaliyolengwa katika mkakati ni pamoja na haya ………

1. Udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe.

2. Udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari; kuwa na madereva wenzabasi-2

3. Uendeshaji magari bila sifa/leseni ya udereva na bima

4. Udhibiti wa usafirishaji wa abiria kutumia magari madogo yenye muundo wa tairi moja nyuma kwa mfano; Noah, Probox

5. Kudhibiti ajali za pikipiki za magurudumu mawili ‘bodaboda’ na magurudumu matatu

6. Abiria kufunga mikanda ya usalama wanapotumia vyombo vya usafiri

7. Kuyabaini na kuyadhibiti maeneotete na hartarishi ya ajali za barbarani ‘black spots/kilometers’

8. Kuangalia uwezekano wa kufanya marekebisho ya sheria za usalama barabarani.

9. Kuanza kwa mfumo wa nukta ‘point system’ kwenye leseni za udereva.

10. Kutoa mafunzo ya msasa yanayolenga katika kuimarisha utendaji wa askari wa usalama barabarani.

11. Kuhakikisha kuwa waendesha bodaboda wanafikiwa na kupewa mafunzo yaa uhakika juu namna na jinsi ya kuzitumia barabara kwa usalama zaidi.

12. Kudhibiti rushwa na kuwaadhibu watoaji na wapokeaji wa rushwa katika barabara zetu nchini.

13. kuwahusisha wamiliki wa magari ya abiria na ya mizigo, katika kuutekeleza mkakati.

14. Kusimamia matumizi ya barabara kwa makundi maalum mfano watoto, wazee, walemavu nawasiotumia vyombo vya moto ‘mikokoteni na baiskeli’

Mkakati mwingine waliouweka ni kuwa Dereva ukikamatwa unapelekwa rumande na baadae mahakamani kujibu shitaka litakalokuwa linakukabili.

Chanzo: Ayo TV

NO COMMENTS