Serikali ya Marekani yalaani wikileaks

0
305

Rais Barack Obama ana wakati mgumu
Tovuti ya Wikileaks, imeanza kuchapisha maelfu kwa maelfu ya nyaraka za siri kati ya balozi za Marekani kuhusu viongozi wakuu duniani na kuelezea mbinu za Marekani za kidiplomasia zinazolenga Afghanistan, Iran na Korea kaskazini.

Baadhi ya mawasiliano yaliyochapishwa ni yale ya mawasiliano kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia na Marekani, pale alipopendekeza vikali kuwa Iran ishambuliwe kijeshi.

Habari hiyo iliyochapishwa na vyombo mbali mbali vya habari hapa Marekani ikiwa ni pamoja na New york Times,Le Monde la Ufaransa,Guardian la Uingereza, Der Spiegel la Ujerumani na majarida mengine yameelezea utendaji kazi wa Marekani katika diplomasia licha ya kuonekana na ulimwengu wakiwa wanapeana mikono na huku wakitabasamu na kupigwa picha. Lakini mwanzilishi wa tovuti ya Wikileaks Jullian Assange, anasema serikali ya Marekani haitaki kuwajibishwa.

Serikali ya Marekani imelaani vikali kitendo hicho na kusema kuwa kitendo hicho kinahatarisha maisha na mabalozi wake.Mtandao huo ulikuwa haupatikani Jumapili na kusema kuwa ulikuwa umeshambuliwa na watu wasiojulikana.

Katika mambo yaliotajwa kuhusu viongozi wengine kama rais wa Italia Silvio Berlusconi kuwa yeye ni kipaza sauti cha Putin huko Ulaya, kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa anakwepa kuchukua majukumu mazito au ya hatari na hana ubunifu, na kwa upande wa kiongozi wa Afrika Muamar Gadaffi kila anaposafiri anasindikizwa na Nesi mwenye uzito kiasi na mwenye nywele nzuri wa Ukraine.

Na wakati huo huo mjumbe mmoja wa baraza la Congress la Marekani kutoka New York Peter King amependekeza kundi la Wiki leaks litangazwe kuwa ni kundi la kigaidi lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa Marekani wanasema hilo litakuwa ni suala gumu kisheria kulitekeleza kwani wao wamepata nyaraka kutoka kwa mtu mwingine.

Naye wakili wa juu wizara ya mambo wizara ya mambo ya nje ya Marekani Harold Koh amesema alimwonya Assange kwamba wikileaks itakuwa inavunja sheria ikichapisha habari hizo lakini Assange akijibu kupitia kwa wakili wake amesema kuwa hana mpango wowote wa kusimamisha utoaji wa nakala hizo.

a

NO COMMENTS