Salamu za Shukrani kutoka Familia ya EX- Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania.

0
564

EAGLE
Familia inapenda kutuma shukrani zetu za dhati kwenu nyote mlioshiriki kwa njia moja au nyingine kutufariji na kutupa nguvu wakati wa msiba na mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Laurence Humphrey Mhomwa aliyefariki tarehe 20 Machi 2015 na kuzikwa tarehe 23 Machi 2015 katika makaburi ya Kinondoni.

Hatuna cha kuwalipa zaidi ya shukrani, tukiwa na imani kwamba Mwenyezi Mungu ndiye atakaewalipa kwa mema zaidi.

Misa ya siku 40 ya kumuombea Marehemu imepangwa kufanyika tarehe 2 Mei 2015 siku ya Jumamosi,

Tunawakaribisheni nyote.

BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

NO COMMENTS