Rafa Benitez apona Inter mabingwa wa dunia.

0
318

Pamoja na kushindwa Jumamosi TP Mazembe wameweka historia ya kuwa timu ya kwanza Afrika kuingia kwenye fainali za klabu bingwa soka duniani huko Abudhabi.

Kocha wa Inter Milan Rafael Benitez alikiri kwamba timu yake ilikuwa na kazi kubwa amesema Mazembe ni timu inayojituma sana na wenye nguvu kimaumbile. Inter Milan imetwaa ubingwa wa soka duniani baada ya ushindi mkubwa wa mabao 3-0, mabao yaliofungwa na Pandey, Etoo na mchezaji wao chipukizi kutoka Ufaransa Biabiany.

Inter walicheza bila mshambuliaji wao hatari Wesley Sneijder kwa sababu ya maumivu lakini alikuwa ni Samuel Etoo aliyepata zawadi ya uchezaji bora wa michezo hiyo na Mbrazil Macon waliotawala mno kipindi cha kwanza. Naye kocha wa TP Mazembe msenegali Lamine Ndiaye ameonyesha kuwa si lazima kuwa na kocha wa nje kuwa na timu nzuri ila uzoefu umeonyesha kuwaangusha timu yake.

Timu yake iliwabana sana Inter katika kipindi pili na kuonyesha kuwa wana uwezo na kumaliza kwa uwiano wa asilimia 44 kwa 56 ya kumili mpira dhidi ya Inter. Nao wachezaji wa Mazembe Kaliyutika na Kabangu wameonyesha uwezo mkubwa na pengine soko lao la nje liko njiani.

Ushindi wa tatu umechukuliwa na Timu ya Brazil Internazional baaada ya kuibwaga Ilhwa ya Korea Kusini 4-2.


Kikosi kizima cha Tp Mazembe.

Kikosi kizima cha Inter Milan mabingwa wa soka duniani.

NO COMMENTS