Polisi waua waandamanaji Ethiopia

0
381

Watu kadhaa wanahofiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya polisi wa kupambana na ghasia kukabiliana na waandamanaji katika mji wa Bahir Dar Ethiopia.

Maandamanano haya yanafuatia yale ya siku ya Ijumaa yaliyoitishwa na wanaharakati kupinga sera ya serekali ya kuwapokonya ardhi kwa lazima ilikufanikisha ruwaza ya taifa ya kuupanua mji mkuuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Serikali ya taifa hilo inakabiliwa na wimbi la maandamano na uasi kutoka kwa makabila mawili makubwa ambayo ndio yanayolengwa na kuathirika zaidi na sera hiyo ya serikali.

Kama ilivyotarajiwa serikali imefunga kwa mara nyingine mitandao ya kijamii kuanzia siu ya ijumaa.

Mwandhishi wa BBC aliyeko Ethiopia Emmanuel Igunza anasema kuwa maafisa wa polisi walilazimika kufyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi hewani ilikutawanya maelfu ya waandamanaji waliofunga mabarabara huku wakimba nyimbo za kupinga serikali.

Waandamanaji hao walijaribu kupeperusha bendera nzee ya Ethiopia katika jimbo la Amhara.

Katika jimbo la Oromia- mamia ya watu wanakisiwa kukamatwa kufuatia maandamanao na makabiliano yaliyoendelea usiku wote.

Serikali imepiga marufuku maandamano yote nchini humo.

Maandamano hayo mwanzo yalianza kwa sababu ya ardhi lakini sasa yanaonekana yanahusu maswala mengi ikiwemo uongozi mbaya wa kiimla ,kukamatwa ovyo kwa vijana kutoka jamii ya Oromo mbali na mauaji ya waandamanaji na wafuasi wao.

Chanzo: BBC Swahili_90705179_582ec25b-1712-4bfc-92b2-d544bc114d4b

NO COMMENTS