Polisi aua wenzake saba Kapenguria, Kenya.

0
615

Polisi nchini Kenya wamethibitisha kuwa mtu aliyeshambulia kituo cha polisi katika eneo la Kapenguria, Kaskazini Magharibi mwa Kenya, na kuua maafisa watano, alikuwa ni afisa wa polisi.

Mamlaka nchini Kenya zimethibitisha kuwa mtu aliyeshambulia kituo cha polisi katika eneo la Kapenguria, Kaskazini Magharibi mwa Kenya, na kuua maafisa watano, alikuwa ni afisa wa polisi.

Maafisa hao waliuawa mapema Alhamisi na mtu aliyeshambulia kituo hicho na kuanza kupiga risasi kiholela.

Polisi wamesema kuwa mmoja wa waliouawa ni afisa anayesimamia kituo hicho (OCS).

Kamishna wa Kaunti ya Pokot Magharibi Wilson Wanyanga alitoa thibitisho kwa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kwamba mshambuliaji huyo alikuwa ni afisa wa polisi.

Ripoti za awali mapema leo ziliarifu kuwa mshukiwa wa kundi la kigaidi la al- Shabab aliyekuwa anazuiliwa katika kituo hicho alimnyang’anya bunduki afisa aliyekuwa akitoa ulinzi na kuwamiminia risasi na kuwaua maafisa wanne.
VOASWAHILI

NO COMMENTS