Papa kuhutubia bunge la Uingereza, watu 5 wakamatwa kwa jaribio la kumuua

0
425
Papa Benedict XVI
Papa Benedict XVI

Papa Benedict yuko Uingereza  katika siku ya pili ya ziara yake ya kihistoria ya siku nne.

 Ratiba  yake ya Ijumaa inajumuisha kikao pamoja na Askofu wa Canterbury Rowan William kiongozi wa kanisa katoliki katika ishara ya kuonyesha  umoja kati ya makanisa hayo yaliyogawanyika.

 Kiongozi huyo wa kanisa pia atatoa hotuba mbele ya wabunge wa Uingereza bungeni kwao.

 Papa alianza ziara yake Alhamisi kwa kukiri kwamba viongozi wa kanisa wameshindwa kuwa makini na wameshindwa kupambana na hali hiyo kwa haraka ya kushughulika na mapadri ambao kwa miongo kadhaa wamewalawiti na kuwabaka watoto kwenye parokia zao.

  Katika misa iliyofanyika nje huko Glasgow Scotland Papa aliwahimiza Waingereza kukataa kutojihusisha na dini na kuonya juu ya hatari za kutohusisha imani za dini katika masuala ya umma.

Wakati huo huo Polisi wa Uingereza wamesema wamekamata watu watano kwa kushukiwa kufanya jaribio la mashambulizi ya uuaji.

Walikamatwa Ijumaa Alfajiri na kusema kuwa wamepanga upya mipango ya ulinzi wa Papa, watu hao walikamatwa huko kati na kaskazini mwa London ambapo Ijumaa  Papa anategemewa kutembelea huko kati kati ya jiji la London.

Lakini Polisi hao walikataa kusema moja kwa moja kama watu hao walitaka kumuuwa Papa Benedicto wakidai uchunguzi bado unaendelea.

Polisi hawajasema nini kilichokamatwa au kupelekea kuwakamata watu hao wakidai bado wanaendelea na uchunguzi.

NO COMMENTS