Pakistan maafa ni makubwa mno kuzidi majanga yaliopita

0
349
Mafuriko ya Pakistan
Mafuriko ya Pakistan

Nchi ya Pakistan imekumbwa  na mafuriko mabaya kuliko yote katika historia ya nchi hiyo kwa mujibu wa Umoja wa mataifa  mafuriko hayo yameleta maafa makubwa kuliko tsunami kwenye bahari ya Hindi 2004, tetemeko la Kashmir 2005 na tetemeko la Haiti 2010 kwa pamoja.

Lakini wachambuzi wanaeleza ni kwa nini  pengine inafikiriwa kama vile  mafuriko haya si makubwa kama ilivyokuwa majanga haya mengine na wameeleza kuwa ni  kutokana na idadi ya watu waliokufa kuwa ni ndogo kuliko hayo majanga mengine.

Lakini kwa mujibu wa Umoja wa mataifa  mafuriko haya ni makubwa sana  kwasababu mpaka sasa idadi ya walioathirika ni kubwa mno  na inaripotiwa  kuwa wanawake wajawazito pekee ni   laki 5  ambao hawana makazi mpaka sasa na karibu watu milioni 13 kwa jumla hawana mahali pa kuishi. Idadi ya vifo inakadiriwa kuwa 1500 mpaka sasa.

Watu wengi wanalala kwenye miti na mahema na wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe. Nchi hii inahitaji msaada mkubwa kwa kweli. Mpaka sasa Marekani imeahidi kutoa dola milioni 150 kusaidia nchi hiyo, lakini hali ya misaada bado inasemekana ni ndogo sana na inapatikana kwa taratibu sana kwani inachukua muda mrefu kuwafikia walengwa.

NO COMMENTS