

Habari zilizotufikia kutoka Mtwara zinaeleza kuwa kumeibuka vurugu ambazo zimepelekea mabomu ya machozi na risasi za moto kutumika baada ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa bungeni na kueleza kuwa mradi wa gesi Mtwara utatekelezwa bila kutaja faida za moja kwa moja watakazozipata wananchi hao. Inadaiwa kuwa kwa sasa kauli mbiu ya wananchi walio katika maeneo hayo ni “Gesi haitoki hata kwa bomba la peni”. Inaelezwa kuwa kituo cha mafuta cha Total kimechomwa moto wakati wa vurugu hizo. Katika kukabiliana na vurugu hizo, inadaiwa polisi kutoka Masasi na Lindi wapo eneo hilo kuongeza nguvu. Taarifa zaidi zitawajia baadae.
MTWARA HALI SIYO SHWARI
Posted in Uncategorized on May 22, 2013 by sunday ShomariBandari ya Dar es Salaam ni kichocheo cha uchumi – Benki ya Dunia
Posted in Uncategorized on May 21, 2013 by sunday Shomari
Tanzania na mataifa jirani ya Afrika Mashariki yanatajwa kuwa yanaweza kuboresha pato la ndani la mwaka – GDP – kama yatachukua hatua za kuboresha ubora wa bandari ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyopewa kichwa cha ‘Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania’ iliyoandikwa na Jacques Morisset, mchumi mkuu wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Uganda na Burundi, Tanzania na majirani zake wanaweza kuongeza pato lao la ndani kwa kiwango kikubwa.
Ripoti hiyo inasema Tanzania inaweza kuongeza pato lake la ndani kwa kiasi cha dola bilioni 1.8 na nchi jirani zinaweza kupandisha pato la ndani kwa dola milioni 830 kwa mwaka, kiwango ambacho kinaelezewa ni hasara iliyotokea mwaka 2012.
Ripoti hiyo inasema kuwa bandari ya Dar es Salaam iko katika njia kuu ya biashara ya Tanzania kwa asilimia 90, na inashughulikia bidhaa zinazogharimu dola bilioni 15 kwa mwaka, sawa na asilimia 60 ya pato la ndani la Tanzania kwa mwaka 2012.Kusoma zaidi bofya Read more »
Suala la Obama kuamua kwenda Tanzania na si Kenya laleta kizaa zaa
Posted in Uncategorized on May 21, 2013 by sunday Shomari
Haya ni majibu ya raia wa Kenya aliyesikitishwa sana na kitendo cha Rais Obama kuamua kwenda Tanzania na kutokwenda Kenya. Aomba Obama asiache kwenda akisema “kwenu ni kwenu acha kuhepa” pia aahidi watampatia zawadi ya kuku akienda huko akaimarket Marekani.
Kuuawa mfanyabiashara Ayoub Mlay, siyo tu kunaacha simanzi bali pia ni fundisho kwa jamii na serikali ya Tanzania.
Posted in Uncategorized on May 21, 2013 by sunday Shomari
Hayati Mlay enzi za uhai wake.
Mlay alifariki dunia usiku wa Alhamisi iliyopita, Mei 16, mwaka huu baada ya kupigwa risasi kwenye Klabu ya Ambrosia, iliyopo Kawe Beach jijini Dar es Salaam.
Simanzi inakuja kwa sababu Mlay, 38, alikuwa mfanyabiashara kijana aliyeonesha mafanikio na kupiga hatua kubwa, amefikwa na mauti akiwa bado na moto wa kusaka maendeleo zaidi kwenye biashara zake na maisha kwa jumla.
Kwa Conrad ambaye ni kijana mdogo pia, anaingia kwenye msukosuko lakini nyuma yake kuna funzo la umiliki na matumizi sahihi ya silaha za moto ambazo kwa sasa zimekuwa kama ‘fasheni’ kwa vijana wengi wa mjini.
WOTE NI WATOTO WA ARUSHA
Mlay ni mfanyabiashara wa Arusha ingawa mara kwa mara hupatikana Dar es Salaam kutokana na mizunguko yake ya kibiashara.
Conrad, naye ni mwenyeji wa Arusha, ingawa kwa sasa makazi yake yapo Dar es Salaam.
Kuhusu kazi ya Conrad, mmoja wa watu waliohojiwa na gazeti hili nje ya Klabu ya Ambrosia, alisema: “Kwa kweli huwa tunamuona, wengi tunamuona ni mtoto wa mjini tu, kwani hatujui anajishughulisha na nini.”
CHANZO CHA UGOMVI
Mtoa habari wetu aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, alisema kuwa Mlay na Conrad ni watu waliokuwa wanafahamiana na kuna jambo walikuwa wanazungumza.
“Siyo rahisi sana kujua walichokuwa wakizungumza ila baadaye yalitokea mabishano. Walitaka mpaka kushikana ili kupigana, watu wakawazuia. Inaonekana Conrad hakukubali, maana aliamua kutoka nje mbio.
“Kwa haraka haikujulikana alifuata nini kule nje, tuliokuwepo tuliamini ameamua kukimbia lakini kumbe alikuwa amefuata bastola. Aliporudi, alikuwa na bastola mkononi, baada ya hapo hata hakutaka kuzungumza maneno mengi, alimpiga Mlay risasi kisha akataka kutoweka,” kilisema chanzo chetu.
WALINZI WALIVYOMDAKA
Chanzo chetu kilibainisha kuwa wakati anapita na bastola kuingia ndani, walinzi walimpisha kwa sababu ya kuhofia usalama wao lakini kipindi cha kutoka, walijipanga kumdhibiti.
Kiliendelea kusema, Conrad akiwa anatoka, walinzi walifanya kama wanampisha na baada ya kupita, walimbana mikono na kumnyang’anya bastola kisha wakamfunga kamba kabla ya kupiga simu kuita polisi.
Dakika kadhaa baada ya kupiga simu, polisi walifika na kufanya mahojiano na watu waliokuwepo eneo la tukio, kabla ya kumchukua mtuhumiwa na kumpeleka Kituo cha Polisi Kawe, Dar es Salaam.
Vilevile, polisi walimchukua Mlay na kumuwahisha Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu, Kinondoni, Dar es Salaam ili akapatiwe matibabu lakini baadaye ilibainika alikuwa ameshakata roho.
ACP Charles Kenyela.
MADAI KUHUSU MATUMIZI MABAYA YA SILAHA
Kwa mujibu mtu aliyejitambulisha kwa jina la Matidau, Conrad alikuwa na mazoea ya muda mrefu ya kuonyesha bastola yake na kuwatishia watu aliotofautiana nao.
“Tunamjua Conrad, kuna watu walishamwonya lakini hakusikia, ikafikia wakati kwamba anapoanza ugomvi, basi tunaomjua tunakaa mbali naye kwa sababu lolote linaweza kutokea.
“Kuna kipindi alinyang’anywa bastola kwa sababu ya tabia yake ya kuioneshaonesha ovyo pamoja na kutishia watu. Tukio hili la mauaji ya Mlay linatufanya tujiulize hiyo bastola alirejeshewa katika mazingira gani au ni nyingine?” kilihoji chanzo.
MINONG’ONO KUHUSU FEDHA
Kuhusu kile ambacho Mlay na Conrad walibishana, kulikuwa na maneno ya pembeni kutoka wa watu waliokuwepo eneo la tukio kwamba chanzo cha ugomvi ni fedha.
“Unajua inapotokea matukio makubwa kama haya, watu wa eneo la tukio wakati mwingine ndiyo huwa wa kwanza kupotosha. Kwa mfano, yapo madai kuwa Mlay alimtuma kazi Conrad, sasa baadaye kukawa na mabishano kuhusu malipo.
“Yote yatazungumzwa lakini jambo ni baya sana. Fikiria kwamba Mlay ni mtu aliyekuwa ameajiri watu, ana familia na marafiki, wote hao wataathirika kwa namna moja au nyingine kwa kumpoteza mtu waliyempenda,” alisema mtoa habari wetu.
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Charles Kenyela alisema kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea na akaongeza kuwa Conrad alimfyatulia Mlay risasi ya kifua.
Kuhusu madai kwamba Conrad ni mzoefu wa tabia za kuchezea silaha na kutisha watu kiasi kwamba hata jeshi lake lina taarifa na liliwahi kumnyang’anya kabla ya kumrudishia kinyemela, Kenyela alijibu: “Hizo taarifa sina, ngoja nizifuatilie kwanza, maana siwezi kuzungumza jambo nisilo na uhakika nalo.
“Nilicho na uhakika nacho ni hiki; kwamba mtuhumiwa tunamshikilia na tutamfikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.”
CHANZO:GPL
Kali TV Online; This week, meet Native Sun
Posted in Uncategorized on May 21, 2013 by sunday Shomari
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Posted in Uncategorized on May 21, 2013 by sunday Shomari
Mei 19, 2013 Chama Cha Mapinduzi kilifanya kikao cha siku moja na wabunge wanaotokana na CCM, kikao hicho kilifanyika mjini Dodoma ambapo pamoja na viongozi wengine wa juu wa CCM kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikao hicho kilikuwa na lengo la wabunge wa CCM na viongozi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye pia ni Rais na mtekelezaji mkuu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kubadilishana uzoefu wa namna ilani ilivyotekelezwa hasa kwenye majimbo kwa kipindi cha nusu ya muhula wa miaka mitano. Baada ya kubadilishana mawazo uliwekwa mwelekeo wa namna bora ya kutekeleza ilani na ahadi mbalimbali kwa kipindi kilichobaki.
Kwahiyo kwa kifupi lengo la kikao hicho ilikuwa ni kutathimini utekelezaji wa ilani majimboni na kuangalia namna bora ya kuweka msukumo mpya na mkubwa zaidi kwa kipindi kilichobaki cha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa 2010/2015, lengo likiwa kuhakikisha ilani na ahadi za CCM na wagombea wake zinatekelezwa kwa kiwango kikubwa.Kusoma zaidi bofya Read more »



