Obama aisifu Kenya kwenye umoja wa mataifa

0
480

Rais Obama akizungumza kwenye Umoja wa mataifa
Rais Obama akizungumza kwenye Umoja wa mataifa
Rais wa Marekani Barack Obama amehimiza suala la amani kati ya Palestina na Israel na kusema amani itapitakana kama Israel ikitambua taifa la Palestina na Palestina kuhakikisha usalama kwa Israel.

Akihutubia katika baraza la 65 la Umoja wa mataifa huko New York Bw.Obama aliuliza ni kwa nini Afrika isiwe msafirishaji mkuu wa bidhaa duniani kwani rasilimali zote ziko huko ,vile vile alikemea mateso wanayopata kina mama wa Congo na kuitaka nchi hiyo kumaliza ghasia za ngono kwa wanawake na suala zima la ubakaji.

Aliisifu serikali ya Kenya kwa kumaliza kura ya maoni kwa amani na kupata katiba mpya. Rais Barack Obama akitoa hotuba Umoja wa mataifa Alizungumzia kuhusu Nyuklia alitoa wito akirudia tena mwaliko kwa Iran kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kuweza kufikia suluhisho la kweli au la vikwazo vitaendelea.

Aliionya Korea kaskazini juu ya vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo, Baraza hilo linaendelea baada ya kufunguliwa Alhamisi huku marais wa nchi zaidi ya 130 duniani wakishiriki mkutano huo. Jumatano rais Obama alitoa hotuba ya kukamilisha siku mbili za mkutano wa baraza la umoja wa mataifa la Maendeleo ya Millenia (MDG).

NO COMMENTS

  1. hilo jengo ni zuri mnoooo. hata kama lime jewnga na wachina hakuna neno. siku moja majengo kama haya yatajewnga na waafrica. wazungu walikuwepo africa miaka mingi mbona hawakujenga lelote la maana.