Obama awakutanisha Netanyahu na Abbas mazungumzo ya ana kwa ana katika miezi 20.

0
365

Rais Barack Obama amefuata nyayo za Rais Bill Clinton na George Bush katika tukio jingine la kihistoria kwa kuwakutanisha mahasimu wawili wa mashariki ya kati Benjamin Netanyahu na Mahmood Abbas  huko White house.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wasuluhishi ambao ni pamoja na Mfalme Abdallah II wa Jordan, Rais wa Misri Hosni Mubarak, Hillary Clinton na mwakilishi maalum wa mashariki ya kati  Tony Blair ambao waliungana na wenzao kwenye hafla ya chakula cha jioni. Mazungumzo hayo ya amani yalianza rasmi  Alhamisi  huko kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani. Haya yatakuwa mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza katika miezi 20. Kwa mujibu wa AFP viongozi hawa wanamisimamo yao kama ifuatavyo:

MSIMAMO WA NETANYAHU:

Netanyahu anataka kuthibitishwa usalama wa nchi yake  na alichaguliwa kwa kuonekana mtu mwenye kutaka usalama na mwenye uwezo na kuonyesha kuwa  si mtu wa mzaha hata kidogo mwenye uwezo wa kutetea taifa la Israel kwa gharama yeyote. Ofisi yake imethibitisha kuwa kizuizi cha muda cha ujenzi kwenye ukingo wa magharibi kitamalizika mwezi  huu kwahiyo ukiangalia wazi suala la kuzuia ujenzi bado kitendawili.

MSIMAMO WA MAHMUD ABBAS:

Yeye si msemaji sana na amekuwa kwa muda mrefu akifanya kazi chini chini akimsaidia hayati Yasser Arrafat katika juhudi zao za ukombozi alipokuwa kiongozi wa PLO mpaka alipofariki akachukua nafasi hiyo. Na alishinda uongozi wa chama hicho lakini  baadaye alishindwa na wapinzani wao Hamas ambao walichukua uongozi wa ukanda wa Gaza na bado Hamas wanapinga mazungumzo haya ya amani na ni wapinzani wa Abbas.  Lakini kikubwa anachotaka ni kusimamishwa kwa ujenzi wa makazi ya Israel huko ukingo wa magharibi ambao kwa sasa umesimama kwa muda tu. Na upinzani alionao kutoka Hamas bado ni kitendawili juu ya ufanisi wake wa suala hili kwa ujumla kwa upande wa Palestina.

MSIMAMO WA OBAMA:

Rais Obama kwa upande wake aliwataka wasipoteze nafasi hii adimu ambayo hutokea mara chache na kuwataka wawezeshe kuwepo taifa la Palestina na Israel iliyo salama na thabiti ndani ya mwaka mmoja. Lakini Obama ameonya kuwa mazungumzo haya hayawezi kuleta mafanikio kwa muda mfupi ukizingatia miaka mingi ya uhasama na  kutokuaminiana na aliongeza kuwa Marekani haiwezi kuyaamulia mataifa haya jinsi ya kutafuta suluhu ila suluhu itatoka kwao wenyewe.

WACHAMBUZI: Darubini ya wachambuzi wengi bado yaonyesha kuwa  kuna kazi kubwa na hali bado ni tete hasa  kutokana na tofauti kubwa zilizopo na pia  kutokuwa na matumaini ya mwenendo mzuri .

mazungumzo ya hali ya juu ya kutafuta amani yalivunjika mwaka 2008  baada ya Israel kuvamia ukanda wa Gaza kwa madai ya kuzuia mashambulizi ya roketi yaliokuwa yakielekezwa upande wake wa Kusini na wanamgambo wa Hamas.

Barack Obama  akiingia white house kwa mazungumzo  na Netanyahu na Yasser Arafat
Barack Obama akiingia white house kwa mazungumzo na Netanyahu na Yasser Arafat

NO COMMENTS