Obama atoa mpango wa kusambaratisha LRA

0
350

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amewasilisha bungeni mpango wa utawala wake wa kuunga mkono kulinyang’anya silaha kundi la Lord’s Resistance Army-LRA, nchini Uganda.

Katika barua yake kwa wabunge waandamizi hapo Jumatano, bwana Obama alisema mpango unatoa muundo kwa Marekani kuhusika katika juhudi za kuwalinda raia na kuondoa vitisho vinavyoletwa na kundi la uasi, ambalo limeongoza kampeni ya vifo na uharibifu kwa miongo miwili.

Mapema mwa mwaka huu, rais Obama alitia saini sheria iliyolenga kuisaidia Uganda na mataifa mengine ya Afrika kupambana na waasi na kuyakamata tena maeneo ya kaskazini mwa Uganda ambako kundi awali lilikuwa makao yake.

Kiongozi wa LRA, Joseph Kony anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu. Anahama hama kuepuka kukamatwa.

Kwa habari zaidi ingia www.voaswahili.comwww.voaswahili.com

NO COMMENTS