Obama atangaza mapambano zaidi na Ukimwi

0
314

Ikiwa leo Desemba 1 ni siku ya Ukimwi duniani rais wa Marekani Barack Obama ameshiriki kushiriki kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani.

Kwa mujibu wa sauti ya Amerika katika tangazo lililotolewa Jumanne Bw. Obama aliahidi kutoa msaada kwa watu milioni 33 wanaoishi na virusi vya Ukimwi duniani. Pia aliahidi upya juhudi zake za kujenga hatua kubwa za maendeleo ya haraka katika mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vya ukimwi.

Jumanne shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limetoa taarifa likisema kizazi cha watoto kinaweza kuzaliwa bila HIV kama jumuiya ya kimataifa itaongeza juhudi za kutoa upatikanaji wa kinga na matibabu ya Ukimwi duniani.

Mpaka sasa kumekuwa na maendeleo makubwa katika mapambano na Ukimwi ambapo watu kadhaa wanaishi na ugonjwa huo kwa zaidi ya miaka 20.

NO COMMENTS