Nigeria yafuzu kwa robo fainali Rio

0
361

Wawakilishi wa Afrika katika kandanda ya Olimpiki ,Super Eagles ya Nigeria wamefuzu kwa robo fainali ya olimpiki mjini Rio baada ya kushinda mechi yao ya pili dhidi ya Sweden.

Sadiq Umar ndiye aliyefunga bao la pekee na la ushindi kwa mabingwa hao wa 1996.

Katika mechi ya kwanza Super Eagles waliwabana Japan 5-4 katika mechi iliyochezwa saa chache tu baada ya kutua Brazil kufutia hitilafu ya usafiri kutoka marekani hadi Brazil.
Nigeria sasa wanajiandaa kwa mechi ijayo dhidi ya Colombia siku ya Jumanne.

Chanzo: BBC Swahili_90711889_78fb64d6-bf3f-4602-8b68-c38e6f78047b

NO COMMENTS