Ngoma Afrika band a.k.a FFU waendelea kudatisha ughaibuni.

0
361

Ngoma Africa band wakifanya yao jukwaani Weserterasse Bremen,ujerumani 7 Nov 2015Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na kamanda Ras Makunja juzi jumamosi ya 7 November 2015 walifanikiwa tena kwa mara nyingine kukonga nyoyo za washabiki mjini Bremen Ujerumani katika onyesho la kusherekea miaka 10 ya Pan African Org. lililofanyika katika ukumbi wa Bugerhaus Weserterasse.Kikosi kazi kazi hiko cha FFU-ughaibuni kikiwa na madansa wao wawili Jessicha Ouyah na Sara Fina waliweza kulimudu jukwaa na kuwadatisha akili washabiki.
Ngoma Africa band ipo katika medani ya muziki kwa takribani miaka 22 sasa na kuweka rekodi ya bendi pekee ya kiafrika barani ulaya inayodumu muda mrefu na kuwanasa washabiki wa kimataifa.
wasikilize at www.ngoma-africa.com

NO COMMENTS