Ne-Yo na mkewe Crystal Smith wanatarajia kupata mtoto wa pili

0
64

Msanii wa miondoko ya R&B duniani, Ne-Yo anatarajiwa kupata mtoto wa pili na mke wake Crystal Renay Smith. Awali msanii huyo alikuwa na watoto wawili aliyozaa na ex wake Monyetta Shaw. Ila baada ya kufunga ndoa mwaka 2015 na mpenzi wake Crystal Renay Smith walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume Shaffer Jr, na kuongeza idadi ya watoto wa tatu kwa msanii huyo.

Taarifa za mkali huyo wa kuimba na kucheza kuongeza mtoto wa nne na wa pili kwa mkewe zimetoka katika mtandao wa kijamii wa Instagram wa Ne-Yo ambapo aliweka picha akiashiria kutoa taarifa kwa mashabiki zake kuwa yeye ni baba kijacho.

‘Guess who having another Baby?’ ndiyo maandishi yanayonekana katika picha aliyokweka msanii huyo.

NO COMMENTS