Ne-Yo amkingia kifua mkewe Crystal Renay

0
423

Baada ya picha ya Ne-Yo kusambaa mitandaoni ikimuonyesha akiwa mtupu, muimbaji huyo ameweka wazi kuwa hajakasirishwa na kitendo alichokifanya mkewe, Crystal Renay kwa kupost picha hiyo.

Muimbaji huyo amesema anafahamu mke wake alimpiga picha hiyo wakati akicheza game, hivyo hakufikiria kuwa angeipost mitandaoni. “Tulikuwa tupo Ohio, na nikuwa nimekaa kwa kurelax na sikufikiria kama mke wangu angepost picha hiyo.Ila nilijua kuwa amenipiga picha,” Ne-Yo amekiambia kipindi cha The Breakfast Club.

Msanii huyo ambaye ni jaji wa shindano la “World Dance” ameeleza pia mipango yake mingine ikiwa ni pamoja na kuachia albamu yake mpya ‘Good Man’ mwezi Septemba mwaka huu.
Bongo5.com

NO COMMENTS