Nafuu njaa ikuue sio nikuletee chakula – Rais Magufuli

0
457

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya watanzania wenye tabia ya uvivu kuwa katika utawala wake hata toa vitu vya bure kwa watu ambao hawataki kujituma kwenye kazi wakisubiri msaada.

Akihutubia wananchi wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga waliohudhuria uzinduzi wa kituo cha mabasi (Stand) wilayani humo, Rais Magufulina amesema kuwa watu wanaopenda kukaa vijiweni bila kujishugulisha huku wakilalamika njaa na hakuna pesa, ni bora wafe na njaa.

“Wakati wa kukaa kwenye magenge na kupiga maneno umepitwa na wakati, mnakaa kwenye pool unasubiri vitakuja hakuna, vya namna hiyo nataka kuwaeleza havitakuja kwenye utawala wangu, mnakaa mnasubiri tuna njaa tunataka mtuletee, mimi njaa nafuu ikuue kuliko nikuletee chakula, kwa sababu kama mwenzako ana chakula wewe una njaa, hatuwezi tukavumilia vitu vya namna hiyo”, amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli amesisitiza kuwa dhamira yake ni kuifanya Tanzania iendelee kwa kusonga mbele kwahiyo hataogopa chochote ataendelea kuongea ukweli hata kama wavivu watamchukia.

NO COMMENTS